Pages

Monday, May 6, 2013

MOVIE REVIEW: KALUNDE

MOVIE: Kalunde
DIRECTOR: Kulwa Kikumba(Dude)
CAST: Irene Paul, Richard Mshanga, Grace Mapunda, Ahmed Ulotu, Hemed Suleiman
RATING: 2/5
Filamu ilianza vizuri kwa story inayomtetea mwanamke kutaka usawa wa kijinsia katika suala la elimu na pia kufanya maamuzi yake binafsi hasa katika suala la ndoa nafasi hiyo ikichezwa na mhusika mkuu Irene Paul aliyecheza kama Kalunde akiwa na ndoto za kusoma lakini baba yake(Richard Mshanga) akimlazimisha kuolewa kwa mwanaume mtu mzima ambaye anajiweza kimaisha(Ahmed Ulotu). Grace Mapunda anamtetea mwanae Kalunde ili apate elimu na suala la ndoa liwe maamuzi yake lakini sio kulazimishwa. Hata hivyo kutokana na mfumo dume uliomtawala baba mtu wanakuwa hawana la kufanya zaidi ya Kalunde kuolewa na Ahmed ulotu ambaye mwanzo alijitia anataka kumsomesha kumbe anamtaka awe mkewe.

Kilichoharibu hii filamu ni story yake kuonekana kuwa na mawazo ya watu wawili tofauti pasipo kujadiliana kwa kina katika mawazo hayo. Story imetungwa na Irene Paul huku Kulwa Kikumba(Dude) ambaye ndiye muongozaji wa hii filamu akiiendeleza story hiyo ambayo kisa kinaisha lakini kama ndiyo kwanza umeangalia part 1 unasubiri part 2. Filamu inavutia mwanzo mpaka kati hasa kutokana na kulijadili suala la usawa wa kijinsia katika elimu na maamuzi huku baadhi ya mistari/dailojia ya Irene Paul na Grace Mapunda ikiwa na nguvu sana katika kumtetea mwanamke huku Irene  Paul akicheza vizuri sana kama msichana wa kijijini mwenye shauku kubwa ya kupata elimu maishani. Hata hivyo baada ya Irene Kuolewa na kwenda mjini story ikakosa mwelekeo, director naye akionekana kupotea licha ya kuongoza vizuri scene za kijijini. Irene Paul naye pia akapotea katika uigizaji kwa kuwa na overconfidence mpaka kuharibu character yake huku matendo na uigizaji wake ukikosa mantiki na uhusiano na mwanzo wa story.

Mavazi ya Irene Paul akiwa mjini kama mke wa mtu tena mzee mtu mzima hayakuwa mbadala. Hemed pia alikuwa kituko katika mavazi utadhani alikuwa anaenda kwenye sherehe au mwanamuziki anayesubiri kupanda jukwaani atumbuize kutokana na mavazi aliyovaa kama mhudumu wa hotel, alionekana wazi kuchemka katika mavazi wakati wahudumu wa kike wakiwa wamevaa sare zao nzuri na za kuendana na eneo husika Hemed hakuleta maana hata kidogo kwa vipuli vyake katika hoteli ile ya hadhi kubwa na nguo zisizoendana na eneo husika. Richard Mshanga aliwekwa mvi ambazo wala hazikuleta maana zikionekana wazi kuwa ni fake tena aliyefanya hivyo akipotea kwakuwa alipogeuka nyuma mvi ziliishia kati kati ya kichwa na maeneo mengine nywele nyeusi tupu, mvi hizo pia hazikuwa na uhalisia wowote.

Kuhusu performances, Grace Mapunda na Richard Mshanga walicheza vizuri katika nafasi zao, Ahmed Ulotu alikuwa kawaida sana. Sudi Ali na Kulwa kikumba walikuwa fresh pia huku Hemed akishindwa kuuva uhusika wake kama kijana mbabe anayelazimisha penzi la Irene Paul. Kama ilivyoelezwa hapo juu Irene Paul alicheza vizuri kama msichana wa kijijini lakini alipogeuka kuwa mjini kama mke wa Ahmed Ulotu acting skills zake zikapotea ghafla na kukosa mvuto katika nafasi yake kutokana na kujiamini kupitiliza na kupelekea overacting.

No comments:

Post a Comment