Denmark kuna wasanii wengi wa filamu wenye asili ya Afrika ambao wanafanya juhudi katika kuendeleza filamu za kiafrika huko ulaya. Solange Chozi Msabaha ni mmoja wao akiwa anaigiza katika filamu za kiswahili zinazotengenezwa nchini humo na kampuni ya VAD Productions. actress huyo tayari amecheza filamu ya Jabuka na Moyo Wangu akiwa na matarajio na malengo ya kufanya vizuri zaidi katika filamu. Solange ambaye alizaliwa Congo na kukulia Tanzania mkoani Kigoma kwasasa ni mwanafunzi wa chuo kikuu nchini humo.
No comments:
Post a Comment