Saturday, May 4, 2013

RJ COMPANY YANUNUA VIFAA VYA KISASA VYA FILAMU.

Rj Company iliyo chini ya waigizaji Vicent Kigosi(Ray) na Blandina Chagula(Johari) imenunua vifaa vipya na vya kisasa katika utengenezaji wa filamu. Kampuni hiyo imekuwa ikijitahidi sana katika suala la picha na mwanga mzuri katika filamu kupitia vifaa vya kisasa lakini licha ya vifaa hivyo bado imekuwa ikizalisha filamu za kawaida huku bado ikikabiliwa na changamoto katika uongozaji wa filamu hizo mara nyingi mhusika mkuu Ray akishindwa kuubeba uhusika ipasavyo kutokana na kushindwa kubadilika kutokana na characters anazocheza, mavazi yasiyoendana na uhusika pia limekuwa ni tatizo kwa filamu hizo. Story pia zimekuwa za kimapenzi mara nyingi kitu ambacho kinatakiwa kuwa kama changamoto ili kampuni hiyo ipate kuzalisha filamu nzuri ndani na nje ya Tanzania kwakuwa vifaa vya kisasa pekee siyo kigezo cha kutengeneza filamu bora na nzuri ingawa matatizo hayo yapo kwa watengenezaji wa filamu wengi nchini.  Kwa upande mwingine  tungependa kuipongeza kampuni hiyo kwa jambo hilo lenye manufaa kwa filamu za Tanzania huku tukiendelea kusubiri suluhisho la hayo makosa mengine. Hongera Rj Company.

                                             images by www.raythegreatest.blogspot.com

No comments:

Post a Comment