Saturday, May 4, 2013

MIMBA YA PENNY YATOWEKA ! AMSHANGAA DIAMOND KUMSINGIZIA KUWA ANA MIMBA YAKE.

Katika hali isiyo ya kawaida mtangazaji Penny ambaye pia ni mpenzi wa Diamond Platinumz amekana kuwa na mimba ya mwanamuziki huyo ambaye aliwahi kukiri kuwa ni kweli Penny ana mimba yake na amempa gari la kuendea clinic ili asisumbuke. akizungumza na mtandao wa Globalpublishers Penny alikana kuwa na mimba ya Diamond na kumshangaa mwanamuziki huyo huku akiwalaumu waandishi kwa kutomuuliza yeye mhusika muda wote huo. Hata hivyo wiki za hivi karibuni habari za kidaku zilianza kusambaa chini chini mitandaoni kuwa Penny ameitoa mimba ya Diamond kwakuwa hamuelewi mwanamuziki huyo. Hata hivyo mpaka sasa bado kujulikana nani mkweli kati ya wawili hao. Ili kusoma mahojiano ya Penny na Globalpublishers ingia hapa www.globalpublishers.info


No comments:

Post a Comment