Pages

Thursday, May 9, 2013

GERMANY KUPITIA ASHLEY TONTO WAUNGANA NA DENMARK ILI KUTANGAZA FILAMU ZA KISWAHILI.

Ashley Toto mwanadada anayetokea Kenya ambaye anaishi Germany kwa sasa anatarajiwa kuigiza katika filamu za Kiswahili zinazotengenezwa nchini Denmark katika kuunganisha nguvu za kutangaza filamu na tamaduni za kiafrika nje ya bara la Afrika. kampuni ya VAD production ya nchini Denmark pia imeambia Swahiliworldplanet kuwa ni kweli actress huyo anayechipukia na mwenye mvuto wa kipekee anatarajiwa kuwa kwenye movies watakazotoa. Ashley mwenyewe alipoulizwa alisema napenda kuwa actress ingawa hii itakuwa mara yangu ya kwanza na ndiyo maana ameamua kuunganisha nguvu za pamoja na waafrika wenzake huko ulaya. Hivi karibuni Ashley alikuwa Denmark akitokea Germany kwa ajili ya issue hizo za kutangaza filamu za kiafrika hasa zinazotumia lugha ya kiswahili. VAD Production pia wamekuwa wakishirikiana kwa karibu na muigizaji Lucy Komba na kwa pamoja wanatarajia kuzindua filamu mpya ya From Tanzania To Denmark hivi karibuni kwasasa mishemishe zikipamba moto kwa sana. More about the actress is coming soon........

                                                             Ashley Toto



1 comment: