Muigizaji maarufu wa filamu Swahiliwood Yobnesh Yusuph(Batuli) amekana habari iliyoandikwa na gazeti moja la udaku la leo kuwa anapokuwa location huwa anapandisha maruhani na haelewi tatizo ni nini kwa kuwa akienda hospitalini wanasema hana tatizo. Gazeti hilo pia limeandika kuwa muigizaji huyo hana anayemshuku kuhusu mambo hayo bali anamuomba mungu amsaidie kuondokana na mambo hayo. Mwandishi wa habari hiyo pia alijitambulisha jina lake na kuweka nukuu za Batuli. Lakini actress huyo ameibuka na kukana habari hizo akisema si za kweli na waandishi wawe makini na taaluma zao wasipotoshe jamii. Kupitia facebook muigizaji huyo sexy Swahiliwood aliandika ................
"Usipotoshe jamii kwa taaluma yako, mnanikwaza sana kwa habari isiyo ya kweli, tumieni kalamu zenu vizuri" huku akiambatanisha na picha iliyotumiwa na gazeti hilo.
Swahiliworldplanet ilipomuuliza muigizaji huyo kuwa mbona mwandishi wa habari hiyo alijitambulisha na kuweka nukuu zako? alijibu "ingekuwa yngu ningekana?". Wiki kadhaa nyuma pia gazeti jingine la udaku linalomilikiwa na kampuni nyingine liliandika kuwa muigizaji huyo ana kansa ya titi katika kichwa cha habari cha gazeti hilo na muigizaji huyo kuibuka na kulaani kitendo hicho cha kumuombea magonjwa mabaya akisema habari hizo si za kweli na zilimsikitisha sana.
Pole mumy ndio umaarufu huo ila hawafanyi vyema.
ReplyDelete