Thursday, April 11, 2013

TAFF NA BASATA TOENI ELIMU KWA FILM PRODUCERS/ACTORS KUHUSU UMUHIMU WA FILM FESTIVALS.

Written by Swahiliworldplanet.

Zanzibar International Film Festival(ZIFF) imedai kusikitishwa na muitikio hafifu wa watengenezaji/waigizaji wengi wa films za kitanzania kutowasilisha filamu zao katika tamasha hilo la kimataifa kitu ambacho ni wazi kuwa watengenezaji wengi wa films Tanzania hawajui maana na faida za film  festivals huku wengine wakiwa na hofu na kutojiamini kuhusu kazi zao wakati wenzao wa Hollywood na Bollywood huwa films zao nyingine zinaanza kuonyeshwa/kuzinduliwa rasmi katika film festivals nchi mbalimbali kabla ya kuingia rasmi sokoni. Ni aibu kwa watengenezaji wa films za kitanzania kutaka tamasha hilo litawaliwe na films za nje na wao wakibaki kushangaa tu halafu eti wanataka wawe wasanii wa kimataifa au kutambulika kama international film makers kutoka tanzania. TAFF ni lazima itoe elimu kwa watengenezaji wa films za kitanzania kuhusu umuhimu wa film festivals maana kuwaachia waandaaji wa ZIFF pekee watoe elimu haisaidii kwa kuwa yapo matamasha mengine kama haya nchi mbalimbali so ni vigumu wao kuja Tanzania na kutoa elimu, lakini TAFF ikiwa na lengo la kukuza tasnia hii itambulike kimataifa inawajibu wa kutoa elimu, sio TAFF tu hata BASATA kama taasisi ya serikali yenye dhima ya kukuza na kuendeleza sanaa nchini inawajibu wa kutoa elimu hii. Hollywood na Bollywoood wamekuwa wakichangamkia sana matamasha haya miaka kibao kwa kuwa wanajua faida zake kwa mtengenezaj husika wa film, waigizaji na film yenyewe. Hata South Africa imekuwa mfano mzuri wa kuchangamkia films festivals. Baadhi ya Faida kubwa za film festivals ni kama ifuatavyo..................

1. Kuunda mtandao wa kikazi(Networking), matamasha haya likiwemo ZIFF hukusanya watu mbalimbali na professionals wa films kutoka nchi mbalimbali hivyo ni rahisi kwa muigizaji au mtengenezaji wa filamu kufanya kazi kimataifa kwa kuwa wataalam wa mataifa mengine wanaweza kuvutiwa na kazi zake hivyo kuingia mikataba ya kikazi.

2. Kukutana na wasambazaji wa kimataifa wa films. wasambazaji wa kimataifa wa films pia huwepo katika matamasha haya wakiangalia vipaji na kazi mpya hivyo producers wa Tanzania wanaweza kupata mikataba mizuri ya kusambaza kazi zao kimataifa na kuepukana na wimbo wa kuwa tunanyonywa na wasambazaji wa sasa.

 3. Kupata tuzo(awards), tuzo ni sehemu ya kujali na kuthamini kazi bora so kitendo cha film, director au actor kupata tuzo kinazidi kumpa thamani na kupaa zaidi ndani na nje ya nchi hivyo kukuza CV yake na mataifa mengine yanayotengeneza films ni rahisi kumfuata ili wafanye kazi pamoja.

4. Kutangaza vipaji vipya. Vipaji vipya hutangazwa katika matamasha haya hivyo kama new film, new director or actor akipata tuzo ni rahisi sana kupata attention kitaifa na kimataifa as an actor or director hivyo kufanikiwa haraka katika kazi zake.

5. Kuzidi kuvutia na kuhamasisha kampuni kubwa za ndani na nje ya nchi ziwekeze katika tasnia ya film. ni wazi kuwa kwa sasa hakuna wawekezaji wazuri kwenye industry lakini kupitia film festivals wawekezaji wa ndani na wa kimataifa ni rahisi kuvutiwa na kuwekeza kwenye tasnia ya film Swahiliwood hasa kwenye usambazaji na production kitu ambacho ni rahisi kuleta mapinduzi katika tasnia hii hasa ukichukulia kuwa utafiti usio rasmi na ulio rasmi tayari unaonyesha kuwa nchi kadhaa ndani na nje ya bara la Africa zinapenda filamu za kiswahili lakini haziwafikii kwa kuwa hakuna wasambazaji wa kuzifikisha huko.

6. Serikali inaweza kushawishika zaidi ikiona kuwa tasnia hii inakubalika na kutoa ajira kwa vijana wengi so itatilia mkazo zaidi katika  kulinda haki za wasanii na hata kusaidia katika maeneo kama vile kupunguza kodi na hata kusaidia kwenye usambazaji ili ikusanye mapato zaidi tofauti na sasa ambapo serikali imejawa na maneno zaidi kuliko vitendo halisi.

7.Kukuza soko la utalii na ku-promote utalii, mara nyingi watalii hupenda kutumia pesa hivyo wakisikia kuna film festival huenda kwa wingi kushuhudia local talents hivyo hununua kazi zinazowavutia na kwenda nazo kwao na huko huzidi kutangaza films husika na hata kushawishi wawekezaji wa kwao waje nchi husika kuwekeza katika tasnia husika.


No comments:

Post a Comment