Friday, April 5, 2013

HONGERA TENA WEMA SEPETU FOR BEING PROFESSIONAL.

Hivi karibuni Swahiliworldplanet haikusita kumpongeza actress Wema Sepetu kwa kumsaidia kumlipia actress mwenzake kajala faini ya mil.13 ili kuepukana na kifungo cha miaka mitano jela. Ila leo tena SWP imeamua kumpongeza tena actress huyo and former Miss Tanzania kwa kuwa more professional. Ni hivi akizungumza na XXL ya Clouds fm Wema alisema amemsainisha Kajala kucheza kama heroine in her upcoming film titled Princess Sasha. Issue hapa siyo kumsainisha bali Kajala kucheza kama leading lady in the movie hii ni kwa sababu  asilimia kubwa ya actors wanaomiliki kampuni za kutengeneza filamu Swahiliwood mara nyingi hujipa uhusika ukuu/main character katika filamu wanazotengeneza hata kama mtu haendani na uhusika wenyewe bali anang'ang'ania kucheza ili aendelee kuitwa muigizaji maarufu aliye juu huku akisita kuwapa nafasi wengine ambao wangeweza kuuvaa uhusika vizuri. Tatizo kubwa hasa likiwa aidha muonekano wa actor kutoendana na character hasa mwili, lafudhi ya muigizaji au general appearance lakini mtu bado anataka kucheza uhusika ukuu sababu ya hofu ya kufunikwa na waigizaji wengine au chipukizi hivyo kuishia kuwapa supporting roles kila mara wakidai hawana bajeti ya kuwalipa waigizaji wakuu!. Hili ni tatizo kubwa ambalo linatakiwa kuondolewa hata kama bajeti zetu ni ndogo but ni vizuri kuangalia kipaji cha mwingine kwa ajli ya kazi bora.

Hii sio kwa waigizaji tu bali hata kwa directors wengine wanalazimisha kuongoza filamu katika matukio ambayo hawana uhakika nayo vizuri badala ya kumpa muongozaji mwingine atakayefanya kazi nzuri ili kutoa kazi bora. Tuige kwa wenzetu. Mfano Director/producer maarufu wa Bollywood Karan Johar licha ya kuongoza films nyingi zilizopata appriciations kubwa kutoka kwa film critics wengi wakiwemo wa Hollywood kama vile films za Kuch Kuch Hota Hai, My Name is Khan, Agneepath na nyinginezo nyingi lakini wakati mwingine anabaki kuwa producer tu na kuwapa kazi ya uongozaji directors wengine wakiwemo upcoming directors. Siyo huyo tu bali huo ni mfano. So kitendo cha Wema kumpa Kajala main Character na yeye kuwa producer hii ni professionalism ambayo Wema ameona Kajala anaweza ku-suit character vizuri kuliko yeye. Pia Wema alisema si kuwa anataka kurudisha pesa alizomsaidia Kajala kwa kumchezesha filamu zake bali atamlipa kama kawaida atakavyolipa wengine kupitia kampuni yake ya Endless Fame Productions.

                                                      Hongera sana Wema Sepetu

No comments:

Post a Comment