Tuesday, April 2, 2013

HII NDIYO FILAMU KWA AJILI YA KUMUENZI KANUMBA TAREHE 7 MWEZI HUU.

Tarehe 7 siku ya Jumapili mwezi huu itakuwa siku maalum ya kumuenzi marehemu Steven Kanumba aliyechochea kukua na kukubalika haraka kwa tasnia ya filamu nchini. Pia kuna filamu mpya maalum ya kumuenzi muigizaji huyo aliyefariki ghafla na kushtua mashabiki wake wengi. Filamu hiyo inaitwa AFTER DEATH(Never happened Before) waigizaji mbalimbali wenye majina wameigiza ili kuungana pamoja kumkumbuka mwigizaji mwenzao. katika filamu hiyo yupo Jackline Wolper, Khanifa Daudi na Patrick Njaidi ambao waliibuliwa na Kanumba na kucheza nao katika filamu ya Uncle JJ na This is It ambazo zilijizolea umaarufu mkunbwa. Pia filamu yake ya mwisho kuigiza ya LOVE & POWER ambayo aliigiza na Irene Paul na Patcho Mwamba itazinduliwa rasmi siku hiyo katika viwanja vya Leaders na kiingilio ni bure hivyo watu wote wanakaribishwa. Angalia kava la filamu hiyo ya kumuenzi Kanumba.


No comments:

Post a Comment