Pages

Monday, April 15, 2013

BONGOMOVIES HAWAJUI KUWA SIMON MWAKIFWAMBA NI RAIS WA TAFF !

Bongomovies ambayo ni club inayoundwa na baadhi ya wasanii katika tasnia ya filamu nchini inaonekana kama haijui au kutofahamu kuwa Simon Mwakifwamba ni rais wa Shirikisho la filamu nchini(TAFF) !. Hii imetokea katika habari waliyoweka katika website yao ya bongomovies.com ambapo walimtafuta Simon Mwakifwamba atoe maoni  kuhusu sakata la Irene Uwoya kudaiwa kulala hotelini na Diamond ilihali Irene ni mke wa mtu. Hata hivyo katika habari hiyo Simon Mwakifwamba alitambulishwa kama muigizaji maarufu na cheo chake cha urais wa shirikisho la filamu Tanzania kikiwekwa kando ilihali mwandishi huyo anaonekana wazi kumtafuta Mwakifwamba akijua wazi ni rais wa sanaa ya filamu nchini hivyo kauli yake ilitazamiwa kuwa ya kiongozi na siyo mtu binafsi. Haikujulikana wazi kama mwandishi alisahau au aliandika huku akijua Mwakifwambwa ni nani hasa ukichukilia kuwa huko nyuma iliwahi kudaiwa TAFF na bongomovies walikuwa katika minyukano ya chinichini. Habari hiyo ya rais huyo wa TAFF kuliongelea suala la Irene Uwoya iliandikwa na mitandao na magazeti nchini huku media na blogs/websites karibia zote zilizoandika habari hiyo zikimuandika au kumtambulisha mwakifwamba kama rais wa wasanii wa filamu nchini. Hatukufanikiwa kupata mawasiliano ya mwandishi wa Bongomovies ili kumuuliza kuhusu hilo ila tukimpata tutakuletea maoni yake. Angalia habari hiyo hapo chini......................

"Baada ya habari iliyotolewa na magazeti ya global publishers kuhusu Irene Uwoya kufumaniwa na Diamond, watu mbalimbali walioongelea suala hilo akiwemo mwigizaji maarufu Simon Mwakifamba ambaye alilaani "vitendo" kama hivyo vya kuchafua tasnia ya bongo movies. bongomovies.com tuliamua kumtafuta simoni mwakifamba ili tupate ukweli wa jambo hilo na hichi ndicho alichokisema, huu ni mtizamo wake tuu. Msikilize hapa kwenye Latest interview na bongomovies.com."

No comments:

Post a Comment