Pages

Sunday, March 17, 2013

KABUTI ONYANGO: KUTOKUWEPO KWA DIRECTORS OF PHOTOGRAPHY IN SWAHILIWOOD NI TATIZO.

suala la picture nzuri katika filamu za swahiliwood bado ni tatizo kubwa kutokana na wengi kutosomea taaluma hiyo na pia kutokuwepo kwa Directors of photography(DOP/DP). Hata hivyo kuna baadhi ya cameramen wanaojitahidi ili kuisogeza tasnia yetu ya films hivyo kutarajia ubora wa picha siku za mbeleni, Mmoja wa cameramen wanaojulikana na ambao tayari wamefanya kazi katika films nyingi ni Kabuti Onyango ambaye kazi zake zinaonekana katika films kama I am Lost, Pusi na Paku, Hekima, Majanga,Chocolate na nyinginezo. Akichonga na swahiliworldplanet Kabuti anasema kuwa alianza kazi ya cameraman miaka 7 iliyopita wakati huo tasnia hii ikiwa changa sana, alianzia katika harusi lakini kutokana na nia yake ya kuwa cameraman mkubwa katika filamu ilimlazimu kutafuta vitabu vya cinematography ili kujifunza zaidi kitaalamu. "nimeanza miaka saba iliyopita na nilikuwa na-shoot harusi tuu sema nillikuwa na nia ya kuwa camera mani mkubwa sana nika jifunza zaidi baada ya hapo nikatafuta vitabu vya cinematography nikajifunza zaidi"

Kuhusu challenges ya kuwa cameraman Kabuti anasema kuwa " changamoto ni nyingi sana kama kukosa dop(director of photography) kwenye kazi zetu then tunafanya kila kitu wenyewe kama sound,taa,nakuwa camera man ni shida bt ndio hivyo tenaaa". Pia cameraman huyo mwenye nia ya kujifunza zaidi ili kazi zake zikubalike zaidi alipoulizwa kuhusu maoni yake kwa upande wa producers alisema "nawashauri maproducer kwamba watuthamin ss camera men". Angalia Kabuti akiwa mzigoni hapo chini............

Kama upo mbioni kutengeneza filamu na ungependa ufanya nae kazi basi unaweza kumtafuta kupitia facebook kwa kufuata link hii http://www.facebook.com/kabuti.onyango?ref=ts&fref=ts




No comments:

Post a Comment