Pages

Thursday, March 14, 2013

DIAMOND AMPA PENNY GARI LA KWENDEA CLINIC, AMUAGIZIA JINGINE JIPYA

Habari ni kuwa Mwanamuziki Diamond Platinumz na mpenzi wake ambaye pia ni presenter Penny wanatarajia kupata mtoto. Kupitia U Heard ya XXL(Clouds fm) Diamond ambaye tayari anakubalika nchi kadhaa kimuziki amesema kuwa amempa Penny gari la kutembelea na pia amemuagizia jingine jipya aina ya Hyundai ix35 ili limsaidie kwenda clinic. "That's true, ni kweli unajua sitaki kusema ni mpenzi wangu, sasa hivi ni mama watoto wangu kwa sababu ya mizunguko ya kwenda clinic na nikaona sio vizuri kwenda kwenye madaladala kugombania......nikaona ni vizuri nikimnunulia gari ya kwendea na vitu vingine. Nimemuagizia ile new model ya Hyundai ix35" . Penny mwenyewe amezidi kuwa mrembo na kuanza kunenepa kuonyesha kuwa kazi aliyoifanya Diamond imekubalika.

Hongera sana kwa wawili hao.

                                                            photo credit: bongo5.com

No comments:

Post a Comment