Tamko
la Marais wa Mashirikisho ya Sanaa nchini
kuhusu
kuagwa kwa
Mhe.
Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Tarehe
19/08/2015 Ukumbi wa Habari Maelezo, Dar es Salaam.
Ndugu wanahabari,
Umoja wa Mashirikisho ya Sanaa
Tanzania unaunganisha Mashirikisho yote ya sanaa nchini kama ifuatavyo:
- Shirikisho la Sanaa za Ufundi Tanzania
(TAFCA)
- Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF)
- Shirikisho la Sanaa za Maonesho Tanzania
(TAPAF)
- Shirikisho la Muziki Tanzania (TMF)
Mashirikisho
hayo yanaundwa na vyama vya wasanii wa fani husika katika ngazi ya kitaifa, yamesajiliwa
kwa mujibu wa sheria na chombo cha serikali chenye mamlaka ya kusimamia
shughuli zote za sanaa nchini BASATA, kilichoundwa kwa mujibu wa Sheria ya
Bunge Na. 23 ya Mwaka 1984 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Umoja
wa Mashirikisho ya Sanaa unachukua fursa hii kuipongeza kwa dhati kabisa serikali
yetu ya awamu ya nne chini ya uongozi madhubuti na uliotukuka wa Mhe. Rais Dtk.
Jakaya Mrisho Kikwete kwa kuonyesha nia njema na ya dhati kwa jitihada zake katika
kuinyanyua tasnia ya Sanaa nchini na kwamba katika kipindi cha uongozi wake
tasnia hii imefanikiwa kukua na kutambulika ndani na nje ya nchi kwa kiasi
kikubwa sana.
Pia
tunawapongeza watu binafsi, Makampuni, Taasisi na Mashirika mbalimbali ya ndani
na nje ambayo kwa namna moja ama nyingine yameonesha nia ya dhati katika kuchangia
kwa hali na mali maendeleo ya tasnia ya sanaa nchini.
Hata
hivyo tunasikitika kuona kwamba kuna baadhi ya watu au makundi mbalimbali kwa
makusudi kabisa wanaitumia vibaya nia njema ya Mhe. Rais kwa kutumia mwamvuli
wa tasnia ya sanaa ambapo huwalaghai wasanii wachache kwa maslahi yao binafsi.
Ikumbukwe
kwamba Tarehe 6/8/2015 kundi la watu waliyojiita Muungano wa Wasanii nchini,
waliandaa tukio la kumuaga Mhe. Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete katika ukumbi
wa Mlimani City huku wakijua kwamba muungano au umoja huo hauko kisheria na
hauna hadhi ya uwakirishi wa wasanii wote nchini.
Umoja
wa Mashirikisho ya Sanaa Tanzania, unatambua haki ya watu au makundi tofauti
katika kuandaa shughuli na matukio mbalimbali likiwemo tukio la kumuaga Rais
wetu mpendwa, kama watanzania walikuwa na haki hiyo. Tunachopinga hapa ni namna ambavyo watu hao wasiyo
na nia njema na tasnia ya sanaa, kutumia mwamvuli wa wasanii wote kinyume cha
utaratibu.
Ikumbukwe
kwamba sanaa nchini ni pana kuliko uwakilishi wa kibaguzi ulifanywa katika
tukio tajwa, kwa mujibu wa tafsiri ya Baraza la Sanaa la Taifa; sanaa
imegawanyika katika maeneo makuu manne kama ifuatavyo:
- Sanaa za Ufundi
- Sanaa za Filamu
- Sanaa za Maonesho na
- Sanaa za Muziki
Tukio
lile siyo tu limekiuka matakwa ya kisheria kwa kutumia jina ambalo halijasajiliwa,
wandaaji kumdanganya Mhe. Rais kwa kujifanya wao ndiyo wawakilishi halali wa
wasanii nchini, lakini pia limeleta sintofahamu na mgawanyiko mkubwa miongoni
mwa wasanii wote wa sanaa zote nchi nzima.
Umoja
wa Mashirikisho ya Sanaa Tanzania, tumesikitishwa sana na tunalaani vikali kitendo
kile na tukiwa ni viongozi halali wa Mashirikisho ya Sanaa nchini na wasemaji
wa wasanii wa sanaa zote tunatamka wazi na tunaomba jumii ya wasanii wa sanaa
zote, wapenda sanaa na maendeleo ya sanaa na watanzania wote kwa ujumla kwamba;
hatulitambui tukio lile na kwamba Mhe. Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amedanganywa
na kwamba bado hajaagwa rasmi na wasanii wote katika Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania.
Tunachukuwa
fursa hii kuishauri serikali ya awamu ya nne na awamu zijazo kuwa makini na
wajanja wachache wanotumia majina ya makundi mbalimbali katika jamii kwa
maslahi yao binafsi, ni vyema Rais wa nchi kama taasisi ikatumia mfumo wa
kiitifaki ambao imejiwekea ili kuwafikia walengwa na kuziba mianya ya wajanja
wachache wanaotumia, ukarimu, ukaribu na nia njema ya viongozi wetu kwa manufaa
yao binafsi.
Umoja
wa Mashirikisho ya Sanaa Tanzania, tunatambua kampeni za uchanguzi zinaanza na
kwa mbinu mbalimbali wasanii watatumika katika kufanikisha kampeni za
wanasiasa, tuna wakumbusha wasanii wasitumike vibaya bali wafanye kazi yao kwa kufuata
maadili ya nchi yetu, weledi mkubwa na kwa makubaliano maalum (Mikataba) walipwe
vizuri bila kudhulumiwa. Tuwaombe watanzania wasiwe na nongwa wanapomuona
msanii amepanda kwenye jukwaa la wanasiasa kwa kumnyooshea kidole, tutambue ya
kwamba sanaa ni kazi kama kazi nyingine na kwamba msanii analipwa kama wanavyolipa
mafundi mitambo na watu wengine katika matukio hayo.
Mwisho
tunawasihi wasanii wote nchini wawe watulivu na wasiyumbishwe na watu wachache wenye
nia ya kutugawa, tudumishe ushirikiano wetu katika kuendeleza harakati za
kupambana na mifumo dharimu iliyokithiri dhidi ya tasnia yetu.
Mungu ibariki tasnia ya sanaa, Mungu ibariki
Tanzania, Ahsanteni kwa kutusikiliza.
Imetolewa na
………………………………………………………………
Kimella Billa
Mwenyekiti wa kamati ya Umoja wa Mashirikiso ya
Sanaa
kwa niaba ya
Marais wote wa Mashirikisho ya Sanaa Tanzania
No comments:
Post a Comment