Friday, August 7, 2015

Interview: Nisha Azungumzia Mambo Mbalimbali Akiwa Nchini China.

Star wa filamu nchini Salma Jbau Nisha kwasasa yupo nchini China kikazi na pia kuangalia fursa za kibiashara. Swahiliworldplanet ilipatana nafasi ya kuzungumza nae mchache kama ifuatavyo...

SWP: .Unaweza kuwaambia kwa ufupi mashabiki wako kuhusu kazi au deal ulilopata china?

NISHA: Kilichofanya nije China ni kujiongezea ujuzi na ufanisi zaidi Wa kazi zangu,na kikubwa nlipata mwaliko kwny chuo cha filamu kilichopo huku nchini China,ikiwa ni moja kati ya ndoto nlizokuwa nazo za siku moja kufika China nikasema nisichezee hii bahati,kwani bongo kuna wasanii wangapi hadi nichaguliwe mm.. Ila kwa kipengele kingine unajua tofauti na sanaa mimi ni mfanyabiashara so nikasema nisije kwa moja..nije kwa yote ikiwemo kujitanua kibiashara zangu.

SWP: .Vipi kwa ujumla maisha ya China na Bongo unayaonaje?

NISHA: Maisha ya China ni mazuri,na kuna vingi ambavyo nimejifunza kwa muda Wa miezi hii nlokuwa huku,ingawa imani kwa WaTanzania ni ndoto sana haswa kwa upande Wa kuvuka border waTanzania walioharibu kwa kukamatwa na madawa ya kulevya wametuponza wengi,maana ikijulikana ww ni mTanzania utaserchiwa masaa utadhani muhalifu..all and I love naipenda Tanzania yng kwa maana haina ubaguzi na ina amani na maisha rahisi muda wote

SWP: Lini unaanza kushuti filamu yako mpya maana kwasasa uko busy China na kazi nyingine

NISHA: Tukijaaliwa nikirudi tu China naanza kushoot,kwa maana kama nlivyokwambia awali nimekuja kuongeza ujuzi na kujifunza mengi nisiyoyajua,tutegemee mabadiliko makubwa ktk filamu zijazo za NISHA'S film production inshaAllah

SWP: Chuo ulichoenda ulijaribu kwenda na nakala za kazi zako za filamu? na walisemaje kuhusu kazi zako kwa ujumla?

NISHA: Yes nimekuja nazo kwani nazo walizihitaji,unajua comedy haikeri kwa namna yyte ingawa hakuna mkamilifu makosa ya hapa na pale yalikuwepo.. Ila na pongezi pia zipo.. kikubwa wamenifunza mengi

SWP: ikifikiriwa Tanzania na China zina uhusiano na ukaribu wa kibiashara je unadhani kazi za wasanii wa Tanzania zikiboreshwa zinaweza kuingia na kuuzika vizuri tu katika soko la China au itkuwa ngumu?

NISHA: Zinaweza kuingia nakuudhika endapo na Wachina wenyewe watajifunza lugha tofauti,kwa maana huku wenzetu lugha yao wameipa kipaumbele sana,wengi wanajua kichina na makabila yao,English wachache sana,labda hapo tuongeze kwny kuweka translation ya kichina kama walivyofanya kirukuu kwa translate ya swahili,..Ila tukijituma zaidi na kuongeza ubunifu wetu tutafika tu

SWP: kwa uliojifunza huko tangu ulipofika ungependa kuwashauri nini wasanii wenzako wa Tanzania kwa ujumla?

NISHA: Ushauri wangu tusijibweteke,tusirudhike kwa tulipo,sio kupata jina na kuonekana kwny filamu mbili tatu tukajiona ndo mwisho nop,inatakiwa tizidi kujifunza zaidi,tujue wenzetu wametupita nn na kwanini wamefika huko,so kutembea nchi mbali mbali zenye kuendelea na kujifunza ni elimu tosha,kwani bila elimu huwezi kuwa na uchanganuo na akili yakinifu ya kujiongeza zaidi..na kufanya vitu vya tofauti..tusiishie tu kuongea kwny interview zetu ohh ndoto zangu kufanya kazi kimataifa,mataifa hayakufati ukilala na kulaza damu anza sasa kunyanyuka kuyatafuta.. tuache starehe zisizo na msingi tutazame future


No comments:

Post a Comment