Thursday, July 30, 2015

Sallai Fatakid Azungumzia Kuhusu Majasiri Na Ujio Wa Kazi Mpya.

Hivi karibuni SWP Planet ilipata muda wa kumuliza maswali Sallai Fatakid ambaye ni msanii aliyejikita katika kumtukuza Mungu nchini Holland. ......

1.Kwasasa wafuatiliaji wa kazi zako watarajie nini kutoka kwako?

SALLAI: Watarajie kuona filamu ya kwanza kabisa kutokea Majasiri(Productions)

2. Filamu itahusu nini kwa ufupi?

SALLAI: Filamu inahusu hali halisi ilivyo kwa sasa kanisani

3.. Na kampuni yako inatengeneza tu kazi za kiroho au hata wanaotengeneza Sanaa za kawaida Kama muziki na Filamu wanaweza kufanya kazi na kampuni yako mfano kukodisha vifaa ?

SALLAI: Majasiri inajihusisha na maswala ya kiroho tu, zaidi ya hapo ni harusi na sherehe zingine za kifamilia zisizotutenganisha na kweli ya MUNGU. Kwa mfano kama siku hizi sisi huitwa kuchukua harusi nk ...

Kuhusu kukodisha vifaa, vikatumiwe na mtu mwingine hapana, ila tu kama anaekodisha sisi tutamfanyia kazi hapo SAWA!

4. Unawezaje kufanya majukumu yote ikiweno Sanaa huku ukiwa baba wa familia ?

SALLAI:
Si rahisi lakini, ni mpango kujipanga . Kila jambo na wakati wake. Wakati wa masomo ni masomo, na wakati wa Kazi ni kazi, Na hii ya tatu kwangu siyo kazi bali huduma ya kujitolea isyokua ya kifaida katika mambo ya kimwili bali kiroho.... Sasa hii ndiyo inayoongoza maisha yote . Maana sasa hii inahusu umilele ambako hauna mwisho, kwaajili ya huko lazima kujitolea yote kwa yote !

5. Baadhi ya washiriki katika filamu zenu hulalamika kuwa mnawabana sana kuhusu kuvaa badhi ya mavazi na mapambo. Je unaweza kulitolea ufafanuzi?

SALLAI: Tunawaomba wote wanaotaka na walio tayari kushiriki kwenye filamu za Majasiri . Kwanza watambue sisi hatuigizi bali tunahubiri kupitia filamu, kwa hiyo hata iweje hatuwezi kuhubiri kuhusu Roho wa Mungu huku tukiwa tumevaa jezi la timu pinzani .Namaanisha hatuwezi kujipamba na kuvaa kama wainjilisti wa dunia na mambo yake kisa eti tunaigiza!.

Huwezi kumkanya au kukemea na kumfundisha kumuhubiri kaka/dada ambae hajaamini au aliepotea kuhusu YESU KRISTO huku mwenyewe ukiwa umevaa na kujikwatua kama wapenda dunia .... Hata kwa hali ya kawaida tu haifai ni kwakua watu wengi wamefungwa sana na niwabishi hata wapendwa wengi kwenye majumba zinazoitwa za ibada . Tumejiwekea mikakati na kutengeneza makubaliano kwa yeyote yule ambaye anataka kuigiza kwetu lazima azingatie .

6.Watu wengi huuliza kama Majasiri ni kundi au...?

SALLAI: Majasiri siyo kundi kama inavyodhaniwa bali ni shirika la kujitolea lisilo la kifaida, karibuni tutawafikia wajane na yatima wakimbizi na makundi kadhaa wa kadha ya watu wasiyo jiweza sana. Hiyo ni kadri jinsi Mungu atakavyotujalia .Amina! Kwahiyo sisi hatupo tu kwaajili ya kuigiza au kushindana kibiashara maana hatufanyi biashara katika huduma hii, tunashughuli zetu tunazozifanya ila hapa ni huduma tu . Tuko tiyari kuchukua video ya nyimbo za kiroho, mahubiri na huduma ...siyo nyimbo, mahubiri na huduma za kidunia zinazojiita za kiroho zilizo lundikana kote. MAISHA katika dunia Ni kama kupanda na kuvuna; apandaye katika mwili Atavuna uharibifu; lakini Tukimtumikia Mwokozi kwa kweli na haki yake yote Tutapata thwawabu mbinguni. Hakuna anaeweza ila tu kuamua na kujikana vilivyo, tungangane hata mwisha maana dunia sasa hata watoto wameona alama za nyakati hizi tulizomo . WAEBRANIA 2 : 1Kwa hiyo imetupasa kuyaangalia zaidi hayo yaliyosikiwa tusije tukayakosa. 2 Kwa maana, ikiwa lile neno lililonenwa na malaika lilikuwa imara, na kila kosa na uasi ulipata ujira wa haki, 3 sisi je! Tutapataje kupona, tusipojali wokovu mkuu namna hii? Ambao kwanza ulinenwa na Bwana, kisha ukathibitika kwetu na wale waliosikia;


No comments:

Post a Comment