Pages

Saturday, December 13, 2014

Zamaradi Mketema Anatafuta Actress Mwenye Sifa Hizi Hapa Ili Kucheza Filamu Yake Mpya.

Zamaradi Mketema ameandika hayo hapo chini kwa hiyo Changamkia fursa..........


“Kwa wale wote wenye ndoto za kuwa WAIGIZAJI WAKUBWA na kama UNA KIPAJI CHA UKWELI hii inakuhusu!!! Ntatangaza rasmi tarehe ya USAILI na MAHALA pa usaili kwa ajili ya filamu MPYA inayotarajiwa kuanza kushutiwa mwishoni mwa mwezi huu ama mwanzoni mwa mwezi unaokuja INSHA'ALLAH!!!
Nafasi ni MOJA tu.. na anaetafutwa hapa ni MSICHANA ambae ndio atakuwa kama muhusika mkuu wa filamu hiyo
VIGEZO:
Asiwe mnene, Awe mwembamba mwembamba kidogo.. Awe DARK SKIN ingawa sio lazima mweusi sana maana wengine wasije wakaogopa.. ingawa hiki sio kigezo kikubwa kama mwili!!! Cha mwili ni muhimu zaidi kizingatiwe... Awe hana matatizo katika matamshi...
Si vibaya akijua hata kingereza cha kuombea maji.. (si lazima FLUENT person) ingawa si muhimu sana pia,
Awe anaongea KISWAHILI fasaha
Cha mwisho ni X-FACTOR!! Ambayo hiyo haielezeki..
Kumbuka tu VIGEZO HIVI si kwa kuamua tu wenyewe ila ni kutokana na sehemu ambayo atacheza ndio imelazimu kuwe na vigezo hivyo!!!
UNAWEZA KUMTAARIFU NA MWENZIO PIA AKAE TAYARI TAYARI!!!
NB: hatutaangaliana usoni atakaechaguliwa atachaguliwa kutokana na kufit hiyo nafasi na akikosekana pia katika hao tutangaza kuwa tumekosa.. though HATUTEGEMEI HILO... kiufupi anaetafutwa hapa ni kama LUPITA LUPITA NYONGO hivi though narudia tena usikariri kwa style hiyo ukakosa kuja kwa kuhofia kumbe wewe ndio tuliokuwa tunakuhitaji!”
Movie yenyewe itaitwa MUKE YA MUZUNGU, Zamaradi alieza;
“MUKE YA MUZUNGU!!!!! kuna visa vingi SANA kwenye hii filamu na ni visa vilivyobeba uhalisia kabisa.. na hata vigezo nilivyovitaja nimevitaja kutokana na visa vilivyopo kwenye filamu hii!!! ARE YOU READY KUIPOKEA!!!!?????? USAILI utafanyika siku ya JUMANNE kuanzia saa SITA KAMILI MCHANA pale LEADERS CLUB... kama kuna mabadiliko yoyote basi itafahamika mapema!!! Namuona kabisa atakaecheza hii filamu atakuwa STAR kiasi gani!! Ikumbukwe tu inahitajika muigizaji wa UKWELI sababu ina vipande vingi ambavyo kama huna kipaji cha ukweli ni ngumu kuicheza!!!”

No comments:

Post a Comment