Pages

Sunday, December 7, 2014

Miss Universe Tanzania 2014 Carolyn Bernad Ang'ara Swahili Fashion Week 2014.

Miss Universe Tanzania 2014 Carolyn Bernad ambaye kwa mara ya kwanza aliibuliwa katika Maridadi Model Search mapema mwaka huu ameonekana kuwa mmoja wa models waliong'ara sana katika Swahili Fashion Week 2014 inayotarajiwa kufikia tamati leo Jumapili katika hotel ya Sea Cliff ,Dar es salaam.

Carolyn amekuwa mmoja wa models waliopata bahati ya kuonyesha designs za wabunifu wengi wa ndani na nje ya Tanzania huku akiwa anawaacha hoi wahudhuriaji wa tamasha hilo kubwa la mitindo wakiwemo wazungu ambapo wazungu wengine hawakusita kumshobokea kupiga nae picha kila anapomaliza shows kutokana na kujiamini kwake na mikogo ya utembeaji wa minato ukiachilia mbali uzuri wa sura na haiba kubwa aliyonayo kama mwanamitindo.

Carolyn anategemewa kufanya vizuri katika mashindano ya Miss Universe 2014 kwa kuipeperusha
vizuri bendera ya Tanzania.

Photos credit: Simon Deiner / Ramp.sdr.co.za

No comments:

Post a Comment