Saturday, December 20, 2014

Inasikitisha Sana Wasanii Wenzetu Kuungana Na Steps Ili Kutuangamiza: Mtitu

Kampuni ya Steps Entertainment Tanzania jana ilitangaza kushusha bei zake za filamu kutoka shilingi 3000 ili ziwe 1500 kwa bei ya rejareja kuanzia mwezi february mwakani.
Hata hivyo suala hilo limepokelewa kwa hisia tofauti na wasanii wengine ambao hawapo chini ya kampuni hiyo na pia kampuni nyingine za usambazaji nchini zimeonekana kutolipokea suala hilo kwa madai kampuni hiyo ipo katika vita kubwa ya kuwapoteza wasanii na kampuni nyingine za usamabazaji nchini ili ibaki peke yake isiwe na mshindani. William Mtitu ambaye ni mmoja wa wasanii wa kwanza kabisa kufanya kazi na kampuni hiyo na baadaye mwaka jana kujitoa kwa madai amechoka kunyonywa licha ya kufanya kazi kwa bidii amejitokeza tena kupinga suala hilo na kuelezea hisia zake. Mtitu aliweka picha hiyo hapo juu ikiwaonyesha Nisha, King Majuto na JB na kuandika...............

"Ama kwa hakika HAWA WAHINDI(STEPS ENTERTAINMENTS) wameamua kutumia wasanii wenzetu kutaka kutuua kibiashara baada ya kuona sasa tumeamua kujikomboa sisi wasanii wa filamu kwa kuamua kusambaza sinema zetu wenyewe baada ya kuwatajirisha kwa muda mrefu nyinyi wenyewe mashahidi marehemu KANUMBA NA SAJUKI WAMEKUFA MASKINI ILI HALI HAWA WAHINDI WANAPATA MAMILIONI
KUTOKANA NA KAZI ZAO MPAKA LEO ,

ANGALIA KÀTIKA HIYO PICHA(INAYOONEKANA HAPO JUU) HAO WOTE NI WASANII WENZETU WANAMSAIDIA ADUI ILI ATUMALIZE, DAH HII INAUMA SANA WATANZANIA WENZANGU .
LAKINI NAWAHAKIKISHIA HIVI VITA LAZIMA TUTASHINDA KWA GHARAMA YEYOTE MAANA HAYA NI MAISHA YETU KWANI WALE WAHINDI BIASHARA YA SINEMA IKIFA WATAUZA SOLAR POWER ,TOYO AU WATAENDELEA NA BIASHARA YA HOTEL YAO YA SUNRISE NARUDIA TENA HIVI VITA LAZIMA TUTASHINDA KWA GHARAMA YEYOTE"

                                                            William Mtitu

No comments:

Post a Comment