Pages

Friday, November 28, 2014

Zitto Kabwe Nimeanza Kurudisha Imani Yangu Juu Yako: Jokate Mwegelo

Mwanasiasa maarufu nchini Zito Kabwe ambaye miezi michache iliyopita wengi walipoteza imani nae baada ya kudaiwa kukihujumu chama chake cha CHADEMA kwa CCM sasa watu wameanza kurudisha matumaini nae tena kufuatia kusimama kidete suala la utakatishaji wa pesa za ESCROW.
Mmoja wa celebrities ambaye awali alipoteza imani na Zito ni Jokate Mwegelo ambaye pia anatajwa kama mmoja wa mastaa walio katika entertainment industry wenye upeo mkubwa wa kuchanganua mambo. Kupitia Instagram Jokate ameandika.....

"Imani yangu kisiasa kwa @zittokabwe imerudi kwa nguvu zote. Jana ameonyesha kwa umma ya watanzania uhodari, jinsi alivyo na uthubutu wa kutetea maslahi ya wananchi at all costs. Tunahitaji wanasiasa wengi wenye kujali maslahi ya mwananchi wa kawaida kabisa wa hali ya chini. Mwananchi ambaye option yake ya matibabu ni hospitali za umma, option yake ya kujipatia elimu ni shule za umma, maisha yake ya kila siku hutegemea sana jinsi serikali itakavyojituma katika kuboresha hizi huduma za kijamii na kadhalika. Zitto Zuberi Kabwe tunamshukuru mama yako kwa malezi aliyokupa alipokuwa duniani yaliyoweza kukufanya uwe mtetezi wa wanyonge na kutufumbua macho sote bila kuogopa pengine hata kuhatarisha usalama wako. I salute you bro @zittokabwe .... Mungu azidi kukuongoza!!"


No comments:

Post a Comment