Pages

Saturday, November 29, 2014

Wema Sepetu Aibua Maswali, Afunguka Diamond Kutwaa Tuzo 3 Channel O Music Video Awards 2014.

Wema Sepetu ambaye wanadaiwa kumwagana na Diamond amempongeza Diamond kwa kunyakua tuzo 3 za Channel O Africa Music Video Awards 2014.
Wema ameandika "Gnyt Instagramers... And Hongera tele ziende kwa kaka platnumz... I must say he did Tanzania proud.."

Hata hivyo kauli ya Wema kwa kuweka neno "kaka" imewatatiza watu kuamini kweli hawapo pamoja kwasasa au wapo katika mkorogano wa kimapenzi.

Katika tuzo hizo Diamond ameambatana na Zari anayedaiwa kuwa mpenzi wake kwa sasa, mama Diamond na management yake. Vile vile watanzania na wasanii wengine akiwemo Vanessa Mdee, Salama Jabiri, Millardy Ayo, Madam Rita na wengine kadhaa wamehudhuria tuzo hizo live nchini S.Africa.

No comments:

Post a Comment