Pages

Friday, November 28, 2014

Nimemuacha Gadner Habash Na Tumeshamalizana: Lady Jaydee

photo credit: Osse Greca Sinare
Baada ya tetesi na fununu kibao kuwa superstar wa muziki wa kizazi kipya Tanzania Lady Jaydee ameachana na Gadner Habash mwanamuziki huyo wa kibao cha Joto hasira ameamua kujimwaga kuwa ni kweli ameamua kumuacha Gadner.
huku akisema kuwa alikuwa akiteswa na kupigwa ingawa hakumtaja moja kwa moja kuwa Gadner ndie aliyekuwa akimpiga. Akizungumza na Times fm katika kipindi cha Sunrise Jaydee alisema

"Kitu kimoja ambacho ningependa watu wafahamu, mimi sio mtu ambaye huwa napenda kuongea maisha maisha yangu kwenye media, kwenye magazeti au wapi, Na ndio maana lolote ambalo linaendelea ndani ya nyumba yangu au kwenye maisha yangu, sijawahi kulitoa nje. Ni watu wanaongea chochote wanachohisi, chochote wanachotaka kusema. Ninavyofikiria mtu anayenipenda mimi alinijua sababu ya muziki na waendelee kuliheshimu hilo, kwasababu kila mtu ana haki ya kuwa na privacy. Ingekuwa kila mmoja angekuwa anatoka kwake anaanza kuelezea mambo yake, mama yake jana walishinda njaa, au mume wake alimfanya hivi, sidhani kama kuna mtu yeyote anapenda kuelezea maisha yake, hata matatizo yake mbele za watu"

Alipoulizwa tena na mmoja wa watangazaji hao kuwa je ameshamtosa Gadner au bado kumtosa Jaydee alijibu "Nimemuacha, Huyu (Gadner) tumeshamalizana"

No comments:

Post a Comment