Monday, November 3, 2014

Mama Wema Afanya Sherehe Baada Ya Wema Sepetu Kumwagana Na Diamond Platnumz.

Wema na mama yake
Hot gossip mpya ni kuwa baada ya madai kuwa Wema amemwaga Diamond Platnumz hivi juzi kati mama Wema Sepetu aliamua kufanya sherehe ndogo ili kujipongeza na kufurahiua Diamond kumwaga.

Chanzo kimoja kikizungumza na Globalpublishers kimesema "Mama Wema alichukizwa kwa kiasi kikubwa na mapenzi ya wawili hao kutokana na kile alichoamini kuwa, Diamond hakuwa na mapenzi ya dhati kwa mwanaye zaidi ya kutegemea nyota yake impe mafanikio ndiyo maana akafanya pati hiyo fupi nyumbani kwake Sinza-Mori, Dar"

Chanzo hicho kiliongeza kwa kusema "Wema hakuweza kuhudhuria sherehe hiyo kutokana na kubanwa na majukumu mengine. Bi mkubwa aliwaita marafiki zake, wakafungua shampeni, wakala, wakanywa na kucheza muziki kufurahia Dangote kupigwa chini"

"Mama Wema chuki zake kwa Diamond hazitaisha kamwe kwa kuwa hampendi tu kutokana na kuona mwanaye hasongi mbele kimaendeleo kama alivyo Diamond ambaye akiachana na Wema mambo yake hayamwendei vizuri kama anavyokuwa na mwanaye"

Mama Wema Sepetu alipotafutwa alisema "Mimi naona huu ndiyo mwisho wa Wema na Diamond na siku zote nasema hakuna uhusiano ukadumu bila baraka za wazazi, niseme tu, sitaki kumuona ndugu yeyote wa Diamond kwangu, kama mahari wakatoe kwa Penny siyo kwa mwanangu"Like our Facebook page Swahili World Planet for more updates about Tanzanian movie stars' latest gossips, news, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news.

No comments:

Post a Comment