Pages

Saturday, November 15, 2014

Mabeef Hayajengi Ningependa Kupatana Na Wema Sepetu: Kajala

Muigizaji maarufu wa filamu Tanzania Kajala Masanja amesema kuwa amefurahi sana Wema na VJ Penny kuondoa beef lao baada ya kupatanishwa hivi majuzi. Akizungumza na Globalpublishers Kajala alisema hata yeye anatamani kupatana na Wema kwani mabifu ni mambo ya kitoto na hayajengi bali yanarudisha nyuma wasanii.

“Hata mimi natamani kupatana na Wema. Mabifu ni mambo ya kitoto sana, kwa kweli nimefurahi sana kuona Penny na Wema wamepatana kwani ni marafiki wa siku nyingi sana na wanastahili ifike sehemu vitu viishe na maisha yaendelee kama kawaida, Hata mimi siku si nyingi tutaweka mambo sawa kwa sababu bifu hazijengi, hazina maana hata kidogo ni kufanya mambo yasiende mbele tu, inabidi tubadilike” alisema Kajala
Wema na Kajala walikuwa marafiki wakubwa kabla ya miezi kibao nyuma kuwa na beef chanzo kikidaiwa ni penzi la mwanaume mmoja hatab hivyo kajala amekiri kuwa beef lake na Wema limechochewa na mashabiki na media pia.

No comments:

Post a Comment