Gossip mpya ni kuwa Wema Sepetu alitokwa na kijasho chembamba baada ya kuziona picha za kimahaba za Zari The Boss Lady na Diamond Platnumz ambaye ni mpenzi wake.
Chanzo toka kambi ya Wema kikizungumza na Swahiliworldplanet kilisema kuwa Wema aliumia kuona picha za Zari naDiamond wakiwa kimahaba akijua ni lazima atakuwa anaibiwa penzi lake hilo kwasababu Zari ni mwanamke mrembo sana na pia mwenye mafanikio kiuchumi akimiliki majumba kadhaa, biashara na magari ya kifahari
"Wema alipoona picha za kimahaba za Zari na Diamond nusura presha impande, yaani jasho lilimtoka si unajua walipotua nchini walilala hoteli moja, acha apate hofu na mali zake unajua Zari ni mwanamke mrembo na mwenye mkwanja wa maana so ilikuwa lazima madam achezwe na machale" kilisema chanzo hicho
Hata hivyo Diamond na Zari mwenyewe tayari wameshasema kuwa picha zilizozagaa mitandaoni ambazo hata wao wenyewe waliziweka zinatoka katika project ya video yao mpya ambayo inatajiwa kutoka katikati ya mwezi ujao. Hata hivyo mashabiki bado hawawaamini wanadhani kuna chembechembe za penzi zinafukuta baina ya Diamond na Zari.
Wala siyo kweli bana wema kamwaga dai muda kabla hata hajaenda south na sasa dai anahaha kumrudsha wema
ReplyDelete