Pages

Friday, November 7, 2014

Busu La Wema Sepetu Na Aunty Ezekiel, Kuachana Na Diamond Ni Fake Ili Kuipa Kick "In My Shoes" Season 2.

Wema na Diamond
Latest news is that, Wema Sepetu na Diamond Platnumz hawajaachana wala nini bali kutangazwa kuachana kwenye media ni mkakati maalum wa kibiashara alioupanga Wema Sepetu na team yake
ya Endless Fame ili kuipigia promo ya kutosha reality show yake ya In My Shoes season 2 ambayo inaanza rasmi leo Ijumaa saa tatu na nusu(21:30) usiku East African television.

Chanzo kutoka kambi ya Wema Sepetu kikichonga na Swahiliworldplanet leo kimesema kuwa Wema hajaachana na Diamond bali kilichofanyika ni mpango maalum ili kuitangaza zaidi in my shoes na hata lile busu/denda alilopigana Wema na Aunty hivi juzi kati ilikuwa mpango huo huo wa kulizima songombingo la Sitti Mtemvu kudaiwa kudanganya umri Miss Tanzania 2014 na hivyo media zote kumgeukia Sitti na kumpumzisha Wema kwa muda.

Wema alipokuwa nchini China hivi juzi kati team yake yake ilimwambia hilo kwa hiyo aliporudi break ya kwanza ilikuwa kwenda moja kwa moja kwenye birthday ya Aunty Ezekiel na kumnyuka busu la haja mbele ya mapaparazi lililoleta maswali mengi vichwani mwa watu ili kutengeneza vichwa vya habari vya magazeti hasa ya udaku, blogs na mitandao ya kijamii.

"Wema na Diamond mbona wapo wote hawajaachana wala nini, ninavyokuambia Diamond ataanza kuonekana katika season 2 ya In My Shoes, lile busu la Aunty na Wema na habari za kuachana na shem wetu(Diamond Platnumz) sio za kweli ni strategies za kuipa kick in my shoes inayoanza leo" Kilisema chanzo hicho

Kiliendelea kwa kusema kuwa Diamond na Wema mpaka sasa hawajaeleza suala hilo kwenye media sababu ukweli wanaujua wao "kwani umewasikia wahusika wenyewe wakisema wameachana?, sisi tunajua kila kitu kama team Wema, kama ingekuwa kweli ungeona fujo zetu Instagram, hakuna la zaidi likiwepo nitakuambia" kilisema chanzo hicho huku kikipekuwa simu yake muda wote

Uhusiano wa Diamond na Wema umekuwa gumzo kwa miaka kadhaa sasa huku wakiachana na kurudiana, wawili hao ambao wamebarikiwa kuwa na umaarufu mkubwa sana nchini bado uhusiano wao haujawahi kupewa baraka na mama Wema ambapo hataki hata kwa dawa Diamond kuwa mkwewe wakati mama Diamond akiwa hana tatizo na Wema kuwa mkwewe.

No comments:

Post a Comment