Thursday, October 30, 2014

Timoth Conrad Uso Kwa Uso Na Ndugu Ya Michael Jackson Nchini Marekani.


image
Timoth Conard akiwa na Tamar Jackson

Muongozaji na muandaaji wa filamu Tanzania, ambaye filamu yake ilifanikiwa kushinda tuzo kubwa za Silicon Valley African Film Festival 2014 nchini Marekani, Timoth Conrad ‘Tico’ ameingia katika rekodi ya kuwa mtanzania wa kwanza kuandikwa kwenye ukurasa wa Facebook wa binamu wa Michael Jackson anayeitwa Tamar Jackson.

image
Post aliyoiweka Tamar Jackson kwenye facebook page yake

Kwenye post aliyoandika Tamar Jackson alieleza furaha aliyonayo baada ya kukutana na Timoth Conrad na kutoa shukurani zake sambamba na kueleza nia yake ya kuambatana na Timoth Conrad wakati atakaporejea nchini Tanzania.

image
Timoth Conrad akiwa na Tamar pamoja na waandaaji wengine wa Filamu nchini Marekani

“Nilijisikia furaha sana baada ya kuonana na dada huyu wa aliyekua msanii mkubwa duniani, sio mtu wa kawaida kwa sababu siku yakukutana nae nilitaka kuzimia maana niliona kama naonana na raisi, sababu alikuja hotelini nilipofikia akiwa na msafara wa magari matatu akiwa ameongozana na aliyekua producer wa baadhi ya nyimbo za Michael Jackson” alisema Timoth Conrad alipoongea na Timamu Habari.

image
Timoth akiwa na Masekretari wake wakati wa kuondoka kuelekea Marekani

Timoth Conrad yupo nchini Marekani hivisasa alienda kwa kushiriki katika tuzo za SVAFF ambapo filamj yake aliyoiandaa na kuiongoza iliibuka kidedea baada ya kunyakua tuzo na kuzibwaga nchi nyingine kama Ghana, Nigeria, South Africa, Malawi na nyingine nyingi.

image
Timoth akiwa ameshika tuzo aliyoshinda

Hatahivyo kulingana na maneno aliyoandika Tamar inaonekana kuwa anampango wa kuja nchini Tanzania.

image
Hapa Timoth akiwa mitaani nchini Marekani

Tuendelee kusubiria kuona nini ambacho kitaendelea baada ya mtanzania mwenzetu kukutana na ndugu huyo wa aliyekuwa mkongwe wa Pop duniani Michael Jackson.

No comments:

Post a Comment