Monday, October 13, 2014

Ray C Amwangukia Zamaradi Mketema, Awapasha Wema Sepetu Na Kajala.

Ray C na Zamaradi
Ray anaonekana kupevuka kiakili na kifikra sana siku hizi ! kupitia mtandao mmoja wa kijamii, star huyo wa muziki wa Bongoflava amewashauri wasanii kuacahana na beef za kijinga badala yake waonyeshane upendo na kuspotiana katika kazi.
Ray C pia hakusita kumuomba msamaha Zamaradi Mketema ambaye walikwaruzana miezi michache iliyopita, huku pia aiwasihi Wema Sepetu na Kajala kuonyeshana upendo kama awali na kusahau tofauti zao
"Kiukweli huwa naumia sana ninapoona mastaa tunatumia muda mwingi kulumbana na kugombana kwa mambo ya kipuuzi sana,mastaa wenzetu wa Nigeria wanatushinda kwa mambo mengi sana sababu wao wanashirikiana na kusapotiana katika mambo mengi sana na hata ukisikia wamepishana basi ujue ni kwa ajili ya biashara tu na si vinginevyo! nilichogundua mimi ni kwamba kumekuwa na makundi mbalimbali mitandaoni yanayokuza mambo na kusapoti wasanii kulumbana mara Team Simba mara Team Nyani! naongea kutoka. Moyoni kuwa watanzania tunasifika kwa kuwa na amani na upendo! sasa iweje tena tuishi maisha ya kuchukiana na ugomvi badala ya kuishi kwa amani?
Najua sisi wasanii tuna mashabiki wengi. na tunawapenda na nyie mnatupenda kwahiyo mnatakiwa kutupatanisha tunapogombana na si kutushabikia coz mnaposhabikia ugomvvi ndio mnapotufanya tupoteze muda kulumbana badala ya kutumia huo muda kufanya kazi zetu za sanaa kwa bidii tutangaze nchi yetu tunapoteza muda kulumbana,wenzetu wanaigeria wako mbali sana kwa sababu wanasapotiana sana! wasanii tuache bifu za kijinga na tutumie muda mchache tuliopewa na mola kufanya kazi zetu kwa bidii tutangaze nchi yetu ili vizazi vijavyo virithi bidii zetu,na naomba sana mashabiki wote msapoti mazuri tuyafanyayo"
Ray C pia hakusita kumuomba msamaha aliyekuwa hasimu wake Zamaradi Mketema ambaye walidaiwa kumgombea Ruge miezi michache iliyopita na kurushiana maneno mitandaoni
"Love u zama n sorry for everything keep doing wat u do best @zamaradimketema n hey dogo langu @wemasepetu and my friend @new_kajala tusameheane na tupendane na tupige kazi Africa watutambue bana!!!!!!"

Like our Facebook page Swahili World Planet for more updates about Tanzanian movie stars' latest gossips, news, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news.

No comments:

Post a Comment