Tuesday, September 23, 2014

Sabby Angel Alikuwa Chaguo La Kwanza Kwenda Big Brother Africa 2014 Kabla Ya Idris Kuchukua Nafasi Yake!

Sabby Angel
Sabby Angel ambaye ni muigizaji wa filamu Tanzania inadaiwa ndiye alikuwa chaguo la kwanza(original choice) kwenda Big Brother Africa "Hotshot" 2014 lakini baadaye Idris ndiyo akachukuwa nafasi yake. Chanzo kimoja ambacho ndicho wiki iliyopita kilichovujisha habari ya majina mawili ya wawakilishi wa Big Brother Africa 2014 toka Tanzania  yaani Irene Veda na Idris wakati kikizungumza Swahiliworldplanet kimerudi tena safari hii kumwaga news kuwa majaji wa auditions walivutiwa sana na Sabby kiumuonekano, urembo wake wa hali ya juu, ucheshi, uwezo wake wa kuchangamana na kila mtu kwa muda mfupi na hata exposure yake wakaona anafaa kwenda pamoja na Irene Veda ila baadaye akachukuliwa Idris

"Sabby ndiyo alikuwa aende Big Brother Africa Hotshot, judges walimkubali sana kuanzia beauty yake, being so friendly and social na drama zake kwa ujumla but even me nikashangaa hajatajwa instead akawa Idris, Irene Veda na Sabby were the original choices, I'm sure hata huyo Sabby mwenyewe hajui hili" kilisema chanzo hicho chenye maneno mengi kikizungumza na Swahiliworldplanet


No comments:

Post a Comment