Thursday, September 11, 2014

Martin Kadinda Ambwaga Wema Sepetu Na Kuwa Meneja Wa Lulu.

Lulu na Martin Kadinda
Habari mpya zisizo na shaka ni kuwa Martin Kadinda kwasasa amekuwa meneja wa star wa filamu nchini Lulu Elizabeth Michael.
Hayo yanakuja baada ya habari kuwa tayari Martin ameacha kazi ya umeneja kwa Wema Sepetu. Akizungumza na Globalpublishers Martin alisema kuwa yeye na Lulu siyo wapenzi bali ni mtu na meneja wake kwasasa na watakuwa wakiambatana pamoja sehemu mbalimbali

“Kwa sasa ‘nammeneji’ Lulu. Naomba ieleweke hivyo ili baadaye watu wasiseme tunatoka kimapenzi kwa sababu nitakuwa naonekana naye kila mara na kwenye sehemu tofauti," alisema Martin ambaye pia ni fashion designer

Kwa upande wa Lulu nae alisema amefurahi kuwa na Martin kama meneja wake
"Huyu ni meneja bora na siyo bora meneja kwa hiyo kama mtu anataka kufanya kazi na mimi, aanze kwa meneja wangu"


 Hata hivyo licha ya Martin kuachia ngazi kwa Wema Sepetu ambapo hivi karibuni alimlaumu kuwa hashauriki lakini kikazi katika filamu hakuna kilichoonekana kwa Wema kuwa alikuwa na meneja zaidi ya kuporomoka na kukosa kazi sokoni.

                                         Martin Kadinda na Wema Sepetu

Like our Facebook page Swahili World Planet for more updates about Tanzanian movie stars' latest gossips, news, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news.

No comments:

Post a Comment