Wednesday, September 17, 2014

Kitendawili, Network, Samaki Mchangani, Kigodoro, Dogo Masai Zapita Mchujo Kuonyeshwa Arusha African Film Festival 2014.

Arusha African Film Festival 2014 ambalo ni tamasha la kimataifa linalotarajiwa kufanyika kwa mara  ya tatu mfululizo kuanzia tarehe 20 mpaka 27 mwezi huu wa September tayari limetangaza majina ya filamu zilizochaguliwa kuonyeshwa katika tamasha hilo la kimataifa ambalo hujumuisha filamu toka mabara yote yaani Africa, Ulaya, Marekani na Asia.
Filamu zilizochaguliwa kuingia ni zile zenye ubora wa kimataifa huku Tanzania nayo ikijitutumua mwaka huu kwa filamu kadhaa zenye ubora kuchaguliwa filamu hizo ni pamoja na Kitendawili(feature), Kigodoro(Feature), Sunshine(Feature), Network(Feature), Little Town Bagamoyo(documentary), Holding Up The Sky(documentary), Samaki Mchangani(Short Film), Rwanda After Genocide(Feature), Dogo Masai(feature), Chizi Karogwa Tena(feature), Mama Africa(short film).

 Filamu hizi za kitanzania zipo sehemu moja tu yaani hazina part 1 na part 2 kuzingatia vigezo vya kimataifa na nyingi zimesambazwa na kampuni ya Proin Promotions ambayo haitaki part 1 na part 2 kujaribu kukuza tasnia ya filamu nchini kuzingatia ubora wa kimataifa. Filamu za Tanzania zenye part 1 na part 2 zimetupwa nje sababu waandaji na wataalamu wa nje wanaziona hazina ubora wa muda katika standard ya kimataifa na vigezo  vinginevyo.

Filamu hizo za Tanzania zitaonyeshwa pamoja na filamu mbalimbali nyingine zilizopita katika mchujo huo toka mataifa mabalimbali ikiwemo Canada, Kenya, Uganda, Austalia, Rwanda, Spain, S.Africa, Guinea Bisau, Brazil, Nigeria, Switzerland, Argentina, UK, Burundi, Morocco. Ili kuona List nzima ya filamu hizo ingia hapa Selected Films Arusha Film Festival 2014.

Pia kutakuwa na tuzo zitatolewa katika tamasha hilo la filamu kwa kazi nzuri.

No comments:

Post a Comment