Monday, September 22, 2014

Cloud Kuanza Maisha Mapya Bila Steps Entertainment.

Cloud
Muigizaji maarufu wa filamu nchini Cloud Issa Musa amesema kuwa sasa ataanza maisha mapya bila kampuni ya Steps Entertainment ambayo kwa muda mrefu alikuwa na mkataba nayo wa kusambaza kazi zake za filamu lakini mkataba huo umefikia ukingoni.
Akizungumza na Vibe Magazine Tz Cloud alisema kuwa anajipanga kuanza kusambaza kazi zake mwenyewe na kutarajia kufaidika zaidi na kazi zake sababu kampuni ya Steps hununua haki zote za msanii ukishapewa pesa kiasi ndiyo hiyo hiyo hupati tena hata kama filamu ikiendelea kuuza miaka na miaka.

Cloud amesema kuwa filamu yake mpya iliyoingia sokoni karibuni ndiyo iliyohitimisha mkataba wake na kumpuni hiyo na kwasasa anajipanga kuja kivingine katika usambazaji wa filamu zake.

No comments:

Post a Comment