Friday, August 1, 2014

Sina Mpango Wa Kuoa Sababu Naweza Kushuka Kimuziki Mapema: Diamond

Diamond amesema kuwa hana mpango wa kuoa kwasasa kwasabu suala hilo linaweza kumshusha kimuziki kwa kupoteza mvuto alionao sasa. Akizungumza na Globalpublishers Diamond alisema........

"Unajua unaweza kuona kama vile nazungumza kitu cha utani lakini ndiyo ukweli wenyewe.
“Kuna wanamuziki wengi walikuwa kwenye peak (kileleni) lakini walipooa tu ‘kiki’ yao ilishuka ghafla katika muziki na wengine wamepotea kabisa"

Ukifuatilia kwa umakini wapo mastaa wengi duniani ambao umri umekwenda sana lakini hawajaoa. Hata hapa nyumbani kuna mifano hai. Nadhani hofu yao ni kuona kuwa wakifanya hivyo watashuka kimuziki,” alisema Diamond.

Diamond alisema hayo huku mastaa wengine wa ndani na nje wakiwa pia na hofu ya kuoa kuogopa kushuka kileleni. Mfano wasanii wengi wa kike Bollywood ni vigumu kuolewa mapema kwasababu inaaminika wanapoteza mvuto sokoni hivyo msanii anajibidiisha kwa miaka zaidi ya 10 akishafika kileleni na kukaa ,muda mrefu anapoanza kushuka mara nyingi akiwa miaka ya 35 ndiyo huamua kuolewa huku wengine mpaka sasa wakiwa na miaka zaidi ya 40 lakini bado hawana watoto wala ndoa, Hata hivyo kwa wasanii wa kiume Bollywood huwa kawaida kuoa na sio rahisi tatizo hilo kuwaathiri sokoni kama ilivyo kwa wasichana. Lakini kwa upande mwingine wachache sana huamua kuingia kwenye ndoa na kuendelea kufanya vizuri sokoni. Suala hili lipo hata Hollywood Kwa hiyo Diamond pengine amealisoma vizuri soko la kazi zake



Like our Facebook page Swahili World Planet for more updates about Tanzanian movie stars' latest gossips, news, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news.

No comments:

Post a Comment