Tuesday, August 19, 2014

Qmobile Tanzania Waleta Mageuzi Ya Huduma Za Matangazo Nafuu Kupitia Simu Za Mkononi

Kampuni ya Quantum Computers Technologies ya Dar es salaam, Tanzania imekuja na huduma mpya za kisasa katika matangazo ya online kupitia simu za mkononi za kisasa. huduma hizo zinapatikana kupitia website yao ya www.m.qmobile.co.tz ambazo ni rahisi na za bei nafuu katika ulimwengu huu wa digital.
Mtu yeyote yule mwenye biashara yake anaweza kuwasiliana nao kujitangaza kupitia huduma zao ambazo zimeanza kupendwa na wengi. Huduma hizo ni kwa biashara yoyote ile na huwa rahisi mtu kungalia huduma hizo popote alipo akiwa na simu yake ya kisasa ambayo baada ya kuingia hapo pia mtu au mteja huweza kuwasiliana na kampuni yoyote ile au mfanyabiashara au mtoa huduma oyote yule kwa kuwa mawasiliano yao huwa hapo.

Pia kama ni mteja mfano anataka huduma toka kampuni au duka flani huweza kuingia kwenye mtandao huo na kuwasiliana na wenye huduma husika ikiwa wao tayari wameingia kibiashara katika mtandao huo. Pia application yake unaweza ku-download baada ya kuingia katika website yao na ina vitu vingi vya kumsaidia mtu ikiwemo ramani ya popote ulipo. Pia huduma za makampuni ambayo tayari wanafanya nayo kazi zipo kwa hiyo uki-download application ya Qmobile Tanzania unapata huduma zao. Mfano kama unataka kwenye Serengeti national park na uantaka kupata huduma zaidi kuhusu wao kama wapo kwenye huduma hiyo absi ukii-download tu unapata habari kamili

Ingia hapa www.m.qmobile.co.tz kupata maelezo zaidi

No comments:

Post a Comment