"Nashukuru kwanza Mungu Muumba wa mbingu na Nchi kwakunipa Uhai, Nashukuru pia Mashabiki wangu Wote wanao ni Support, Wanao Nikubali naku Kipenda kipaji changu Nakuzikubali kazi zangu, Napenda kudhihirisha furaha yangu kwenu mashabiki wangu kwaku wajibu nakuwaambia Malengo yangu katika filamu baada ya miaka mitano Ijayo, nina malengo mengi sana ispokua zipo za muhimu, Kwanza Nitapambana na niliisha anza kupambana ili Filamu zetu za kitanzania Ziwe za kimataifa zaidi,Nakuhakikisha Soko la filamu linaeleweka vizuri, Ma-Producer na Wasanii wapewe haki zao kama Wasanii wa Nje,
Pili: Napigania sana Kutetea haki za wasanii chipikizi kwasababu wana nyanyaswa sana, Hawapewi thamani kama wasanii haswa, Wanaonewa, Wana Nyanyaswa, Hawa thaminiki,Nilazma Nitumie nguvu nyingi kwaku ungana na Wenzangu Wenye Uchungu Kama wa Kwangu ili katika miaka yambele tulingane wote, Mwisho kabisa, kuna msemo usemwao kuwa msahau kwao ni mkimbizi, Sasa mimi sitaki niwe mkimbizi, Nina malengo yakui inua Congo pia katika Swala nzima la filamu, Jinsi tunavyo tambulika Dunia nzima kimziki, Basi hata ki filamu Congo ijulikane pia kuwa inaweza, Natayari nilisha anza hio mikakati ili kufanikisha swala hilo, Kubwa zaidi Mashabiki wangu waendelee kusubiri vitu vipya kutoka kwangu, kila filamu watakayo Sikia nimeshiriki au Nimetengeneza basi watarajie kuona vitu vipya vyenye Ubora wa Hali ya Juu."
Like our Facebook page Swahili World Planet for more updates about Tanzanian movie stars' latest gossips, news, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news.
No comments:
Post a Comment