Saturday, August 16, 2014

Irene Paul Amchana Steve Nyerere Kwa Tukio La Kuwaombea Wasanii Waliofariki Kwa Maslahi Binafsi.

Irene Paul
Leo kuliandaliwa tukio la kuwaombea waigizaji mbalimbali wa filamu nchini walioaga dunia tukio hilo likiongozwa na mwenyekiti wa Bongo Movie Unity Steve Nyerere.
Hata hivyo inadaiwa kuwa Steve ameandaa tukio hilo kwa maslahi binafsi na sio nia ya dhati kuwaombea wasanii hao waliotangulia mbele za haki. Vile vile inadaiwa tangu juzi usiku na jana baadhi ya wasii wa kundi hilo walikuwa wakitumiana sms ili wasihudhurie issue hiyo kwa madi siyo kabisa. Mitandao ya kijamii nayo haikuwa nyuma kulaani kitendo hicho. Sasa Irene Paul aliye star mkubwa wa filamu nchini Kupitia Instagram nae ameandika ....

"KWELI KUFA NI KUFAANA, laiti waliotangulia wangejua yanayoendelea kwa majina yao mbaya zaidi waliofiwa wanaona wanasaidiwa wakati ni haki yao kwa HESHIMA waliyopewa na wapendwa wao kwa njia moja au nyingine, LAITI michango inayotolewa kwa majina yao ingetumika kwa familia zao hata wakiitumia vibaya ni wao KULIKO watu baki sababu ya unyonge wao, ingekuwa la maana tungewaombea MOYONI kila siku kwa mapenzi ya DHATI na si kwa siku moja kwa sababu fulani binafsi hasa kimaslahi, TUNAPITA HATUJUI KESHO YETU MASKINI, LAITI tungalijua tungetengeneza leo yetu kwa ajili ya kesho yetu,IT'S MY DAILY PRAYER THAT MUNGU ATUPE HEKIMA YA KUMJUA YEYE ZAIDI maana kwa njia hiyo pekee itakuwa salama yetu na atatuepusha na shari nyingi ambazo zitatuelekeza ktk kheri nyingi tukiwa hai na tukienda#ASANTEMUNGU#🙏🙏 myownthinking#myownwords#justhoughts#fikrazangumwenyewe#manenoyangumwenyewe#☺"

                                                          Steve Nyerere

No comments:

Post a Comment