Friday, July 25, 2014

Steve Nyerere Anusurika Kuvamiwa Na Watu Waliotaka Kumdhuru.

Muigizaji wa filamu na mwenyekiti wa kundi la Bongo Movie Unity Steve Nyerere jana alinusurika kuvamiwa na watu wasiojulikana waliotaka kumjereuhi wakiwa na mapanga. Bahati tu kulikuwa na watu nyuma yake ambao waliwahi kumtaarifu asishuke ndani ya gari. Kupitia Instagram Steve aliandika

"Eeeee Mungu leo nilikuwa na kikao cha PSPF asubuhi, jioni ndugu yangu rafiki Devis Mosha akatualika kwake baadaye nikawa na wageni wangu toka Shinyanga wakati narudi home nilizingirwa na gari mbili nakulazimisha nishuke bahati nzuri ikapita gari ambayo watu wananijua na kuniokoa, Mungu nioke baba"

Pole sana Steve kwa masahibu hayo Mungu akulinde...

Like our Facebook page Swahili World Planet for more updates about Tanzanian movie stars' latest gossips, news, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news.

No comments:

Post a Comment