Saturday, July 26, 2014

Photos: Happy Nyatawe Aja Na Vitu Vikali.

Star wa filamu anayefanya vizuri katika filamu mbalimbali Happy Nyatawe ameingia katika biashara ya nguo, viatu na vitu vinginevyo vya fashions ikiwa kama sehemu ya kujitanua kiuchumi. Hata hivyo Happy amesema kuwa kamwe hawezi kuacha kazi yake ya uigizaji kwani ipo kwenye damu yake na anaipenda sana.

"niliogopa biashara lakini sasa naifurahia biashara yangu sana ninamshukuru Mungu nimethubutu na nimeweza, nakumbana na mambo mengi kama kugombana na watu na ajali njiani ila mwisho wa siku napata changu, Wapo wastaarabu na wanaodharau biashara yangu lakini nashukuru sitegemei kuomba, Nauza pich .raba tishet na gauni na simple shoes, nimefundua pesa yakuhangaika mwenyewe ni tamu na inauma pia, nimegundua pesa ya kutafuta mwenyewe ni tamu na inauma pia. Na biashara yangu hainizuii kufanya kaz zangu za movie, Nafanya na sijaacha wala sitegemei kuacha" Alisema star huyo wa filamu za Zena na Betina na Baamedi

Zinazoonekana ni baadhi ya nguo na viatu anavyouza Happy akiwa yeye mwenyewe kama model wa ingizo lake jipya kwa hiyo ukitaka kununua basi wasiliana nae hapa Happy Nyatawe 0713659864
 ili na wewe upendeze na kwenda na wakati..........

No comments:

Post a Comment