Pages

Sunday, June 1, 2014

Wasanii Mbalimbali Waupokea Mwili Wa George Tyson Katika Hospitali Ya Kairuki, Dar

Mwenyekiti wa Bongo Movie Unity Steve Nyerere, akiwasili katika Hospitali ya Kairuki kusubiri mwili wa marehemu. Steve alivalia tisheti yenye ujumbe 'Why always me'.
Mke wa marehemu Tyson, Beatrice Shayo akiwa na simanzi wakati akiusubiri mwili wa mumewe.
Dada wa marehemu Tyson, aitwae Doreen akisubiri mwili wa kaka yake.
Ni majonzi kwa kila mmoja aliyefika kuusubiri mwili wa marehemu Tyson Hospitali ya Kairuki, Mikocheni, Dar.
Msanii wa filamu  Kelvin akihojiwa kuhusu alivyopokea taarifa za kifo cha mwongozaji filamu, George Tyson.
Mtangazaji wa Kipindi cha Wanawake Live kinachoruka kwenye runinga ya EATV, Joyce Kiria akilia kwa uchungu.
Mwigizaji Aunt Ezekiel naye alikuwepo kupokea mwili wa Tyson.
Wema Sepetu akihojiwa na mwanahabari wakati wa kupokea mwili wa Tyson.
Mwenyekiti wa Bongo Muvi, Steve Nyerere akibadilishana mawazo na mmoja wa waombolezaji.
Mlinzi wa mochwari katika Hospitali ya Kairuki akiusubiri mwili wa Tyson.
Waombolezaji wakiwa wamebeba jeneza lenye mwili wa George Tyson kuupeleka mochwari.
Jeneza lenye mwili wa George Tyson likiingizwa mochwari katika Hospitali ya Kairuki, Mikocheni jijini Dar.
Mwili wa Tyson ukiwa mochwari katika Hospitali ya Kairuki.
Dada wa marehemu Tyson, Doreen akilia kwa simanzi baada ya mwili wa kaka yake kuwasili.
...Doreen akiwa amepoteza fahamu baada ya mwili wa kaka yake kuwasili Hospitali ya Kairuki.
Gari lililobeba mwili wa marehemu Tyson, aina ya Toyota Land cruiser lenye namba za usajili STK 6630 kutoka Wilaya ya Mvomero likiwasili Hospitali ya Kairuki kutoka mkoani Morogoro.
...Gari hilo baada ya kuwasili na mwili wa Tyson.
Mastaa wa filamu, Rose Ndauka (kushoto) na Jack Pentzel wakiwa Hospitali ya Kairuki kuupokea mwili wa Tyson.

Mr. Chuz akielezea alivyoupokea msiba wa George Tyson.
(Picha zote na Gabriel Ng’osha/GPL)

No comments:

Post a Comment