Pages

Friday, May 30, 2014

Breaking News: Muongozaji Wa Filamu Nchini George Tyson Afariki Dunia Kwa Ajali Ya Gari.

George Tyson
Tasnia ya filamu nchini imepata pigo jingine baada ya muongozaji wa filamu wa siku nyingi George Otieno Tyson kufariki dunia kwa ajali ya gari maeneo ya Morogoro akitokea mkoani Dodoma. Inasemekana katika ajali hiyo alikuwa na watu wengine. Katika enzi za uhai wake Tyson alikuwa mmoja wa waongozaji wa kwanza wa filamu na michezo ya runingani nchini huku akiwa amechangia kuwainua wasanii kibao wakubwa sasa akiwemo Yvonne Cherryl "Monalisa" ambaye waliwahi kufunga ndoa kabla ya kutengana huku wakiwa na mtoto mmoja wa kike. Tyson pia aliwatoa mastaa kama Hemedy kupitia filamu kama Who Is Smarter. Nae Monalisa ameonekana kushtushwa na kifo hicho na kupitia Instagram ameandika "George, u were my 1st director, then my friend, you became my lover, then hubby, then the father of my 1st born Sonia Akinyi, then you turned out to be my enemy, then back to my best. leo umeniweza. Sonia your Angel as you always call her haamini hadi sasa, nalia kwa nguvu, nalia moyoni, nina maumivu ya ajabu. R.I.P George Otieno Okumu"

Gari lililopata ajali
Tyson katikati akiwa na Jokate na Ezden wakati wakiandaa kipindi cha The One Shiow
Vile vile Tyson alikuwa muongozaji wa kipindi cha The One Show kinachorushwa TV1 ambacho kwa muda mfupi tu tayari kimejipatia umaarufu huku watangazaji wake wakiwa Jokate na Ezden. Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi. Ameen

No comments:

Post a Comment