Dida na Ezden |
"Mimi na mume wangu huwa hatuna mipaka katika simu zetu, kila mtu yuko huru kuchezea simu ya mwenziye. Siku ya tukio jamaa (Ezden) kabla hajaenda kuoga alitengeneza namba za siri (pasword) sasa nilivyotaka kucheza gemu nikamfuata bafuni na kumuuliza mbona simu imefungwa, nikamuomba anifungulie, huwezi amini akaanza kunitukana, nikajiuliza ni simu tu au kuna mengine" Alisema Dida ambaye alitamba na tamthilia kadhaa za Kaole
Aliendelea kwa kusema "“Nilishangaa sana, nikajiuliza kosa langu ni nini? Alinipiga hadi akanipasua sehemu ya kichwa, sikuamini kama Ezden anaweza kunifanya vile au kama alinichoka angeniambia wakati yeye ndiye mkosaji"
Dida amesema kuwa anachotaka sasa ni talaka yake na alishindwa kumuomba mumewe huyo msamaha siku ile ile. Ukiachilia mbali ndoa hii ya Dida iliyo kitanzini, huko nyuma alifunga ndoa na Mohamed Mchopanga na Gervas Mbwiga "G" na kisha wote kumuacha kwa talaka.
Dida na Ezden |
No comments:
Post a Comment