Pages

Friday, June 13, 2014

Monalisa Afunguka Kwa Uchungu Kufuatia Maneno Kuwa Hakustahili Pole Za Msiba Wa George Tyson.

Monalisa
Star mkubwa wa filamu Swahiliwood Yvonne Cherryl " Monalisa" ameamua kufunguka kwa uchungu kufuatia baadhi ya watu kumsema kuwa hakustahili pole za aliyewahi kuwa mumewe na muongozaji wa filamu na michezo ya kuigiza George Tyson aliyefariki wiki kadhaa nyuma na kutarajiwa kuzikwa Jumamosi hii huko Kenya. Kupitia Instagram Monalisa ameandika.......

 "let me clear the air.. ni hivi pamoja na ujinga tulioufanya mimi na George katika maisha yetu, kwa macho ya kibinadamu utasema alikuwa na mke mwingine but kwa macho ya ki-Mungu mimi ni mke halali wa George Otieno Okumu aliyelala, anasema mke wa Tyson alijifungua ndani mimi nikawa nachukuwa pole zisizo zangu, dah! kwanza wanawake walikuwa wawili ndani sio mmoja na wote walijifungia ndani, kwanini? jiulize kabla ya kuropoka halafu wewe ni mwanamke kuna siku yatakukuta, nilienda kutimiza wajibu wangu kama mke, ningelia peke yangu kwetu mngesema sana, nimekaa msibani naambiwa nachukua pole za bure, wacha nikukumbushe maandiko....alichokiunganisha Mungu? ....kilichofungwa 

duniani......nikupende nikutunze hadi kifo?........sasa kifo kimetutenganisha, siku ya mwisho unadhani George ataitwa na nani? pamoja na mambo yake yote acheni nimlilie he was a good father kwa Sonia wangu especially miaka 5 ya mwisho wa uhai wake acheni nimlilie he was my bestfriend 1998-2014, nime-share nae kitanda 2000-2006 nitakuwa mtu wa aina gani nisiwe na uchungu? ukiona mwanamke mwenzio kaishindwa ndoa usimcheke jua kuna sababu...na ni fundisho lwa wachukua waume za watu wote mjini. mume akiumwa huwa anarudi kwa mkewe na akifa? and for your info....msianze anajifanya mke sasa hivi ili apewe mali.....Sonia ni mali kubwa sana aliyoniachia so am happy waache wao wanaolilia kupewa pole wapiganie, mwenyewe aliyetafuta kafa kaziacha sembuse tuliobaki ? niacheni nimlilie, waacheni fans wangu walie na mimi"
Monalisa

Like our Facebook page Swahili World Planet for more updates about Tanzanian movie stars' latest gossips, news, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news.

No comments:

Post a Comment