Pages

Friday, May 30, 2014

Steve Nyerere Na Baba Haji Nusura Wazichape Kisa Steve Kumtaka Baba Haji Amchunie JB Msibani.

Steve Nyerere
Muigizaji wa filamu nchini Haji Adam 'Baba Haji" na mwenyekiti wa Bongo Movie Unity Steve Nyerere ambaye pia ni muigizaji nusura wazichape kwenye msiba wa msanii mwenzao Rachel Haule. Tukio hilo lilitokea huko Sinza, kwa mujibu wa chanzo kimoja kikizungumza na Globalpublishers Steve alimwambia Baba Haji amchunie JB na asiwe karibu nae bila Baba Haji kujua sababu za msingi kwanini amchunie JB bila sababu ndipo wakataka kuzichapa bahati William Mtitu akawahi kuwaamulia "Hata haikujulikana kwa nini Steve hakutaka Baba Haji awe karibu na JB, akammaindi ndipo mtiti ulipoibuka, wakataka kushikana mashati bahati nzuri Mtitu (William) akawaamua" kilisema chanzo

Steve Nyerere alipouliwa na mtandao huo hakujibu chochote ila Baba Haji ambaye ni msanii wa muda mrefu anayetamba na filamu kibao sokoni kwa mshangao alisema "Sijui jamaa vipi, au ananionea wivu, nashindwa kumuelewa"
Haji Adam "Baba Haji"
Wiki iliyopita pia Steve nyerere alidaiwa kueneza sumu kwa mastaa ili wamchunie JB na William Mtitu baada ya kudaiwa kutofautiana  nao kauli msibani hapo. Ukiachilia hilo Steve Nyerere hivi karibuni alimshutumu JB kuwa aliwachagua wasanii wake kwa safari ya kwenda Uturuki bila kuwashirikisha, safari hiyo ilidhaminiwa na Princess Casino ingawa JB alikatisha ziara hiyo baada ya kifo cha Kuambiana. Wiki kadhaa nyuma pia msanii mmoja alikaririwa na gazeti moja akimshutumu Steve Nyerere kuwa na mabifu ya sio na maana na wasanii wenzake na kutaka wengine wawachunie watu anaogombana nao.
                                                            JB
Like our Facebook page Swahili World Planet for more updates about Tanzanian movie stars' latest gossips, news, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news.

No comments:

Post a Comment