Pages

Friday, May 30, 2014

Mnikome Situmii Mkorogo, Bali Nina Asili Ya Afrika Na Uarabuni: Sabby Angel

Sabby Angel then and now
Muigizaji wa filamu ambaye pia ni mwanamuziki chipukizi Sabby Angel amewakoromea wale wanaomzushia kuwa anatumia mkorogo kwa kusema kuwa weupe wake ni wa asili kwani wazazi wake wana asili ya uarabuni na Africa kwa hiyo yeye ni chotara wa kiafrika na kiarabu. Pia kupita page yake star huyo wa filamu ya Hard Price ameandika maneno hayo hapo chini na kuweka picha yake ya utotoni akiwa mweupe kama sasa.

  "Kwa wale wanafiki wanaosema madam Sabby Angel napaka mkorogo kuwa mweupe picha hiyo hapo ya nikiwa mdogo sasa ! acheni unafiki kwa mambo msioyajua, kama una tatizo na Sabby kasage chupa unywe, tafuteni lingine la kusema mahasidi vidudu watu, msione mtoto wa watu napendeza na kufanikiwa, Sabby Angel ni original African beauty na sio copy and paste kama mlivyozoea, mapepo nyie mshindwe
Sabby Angel

No comments:

Post a Comment