Wednesday, May 7, 2014

Skyner Ally Apata Mtoto Na Nay Wa Mitego.


Skyner Ally
Ile ndoa iliyofungwa kwa mbwembwe na kuvunjika kabla ya mwezi mmoja kati ya msanii wa filamu nchini, Skyner Ally na Saad Omar, chanzo ni mwanamuziki wa Bongofleva Nay wa Mitego’.

Nay Wa Mitego
Habari za awali zilisema kuwa, ndoa ya Skyner iliingia mdudu baada ya mumewe kugundua kuwa alinunua ‘mbuzi kwenye gunia’, kwani bidada huyo alikuwa na ujauzito wa mtu mwingine.
Hata hivyo, minong’ono ilikuwa inasema kuwa, mimba hiyo ilikuwa ya Nay ingawa awali, hakuna aliyekuwa tayari kufafanua kuhusiana na ishu hiyo.
Ndoa ya wawili hao ilifungwa Oktoba 7, 2011 nyumbani kwa dada yake, Magomeni – Mapipa, Dar es salaam na kufika tamati kabla ya mwezi Novemba, dah!
Ripoti zinaonesha kuwa, baada ya Skaina kutemwa na Saad alimweleza Nay sababu na kutimkia kwao Iringa ambapo alipojifungua alimweleza ukweli mwenzi wake huyo kuhusu ujio wa mtoto wao.
Wawili hao wameelezwa kuwa na mawasiliano ya karibu lakini ya siri kwa muda mrefu ila hivi karibuni, wote waliamua kuutua mzigo huo na kuweka mambo hadharani ambapo kwa upande wa Skyner alisema: “Nadhani mmechelewa tu kujua, lakini habari ndiyo hiyo.”
Skyner
Nay alipoulizwa, alijibu kwa kifupi sana: “Ni kweli lakini ni mambo ambayo huwa sipendi kuyazungumzia sana.”
Ili kuthibitisha ukweli huo, wikiendi iliyopita, baada ya Nay kutwaa tuzo moja ya Kili katika kipengele cha Wimbo Bora wa Kushirikiana, Skyner alitupia maneno ya kumpongeza Nay katika ukurasa wake kwenye Mtandao wa Kijamii wa Instagram yaliyosema:
“Hongera baba mtoto wangu kwa kuchukua tuzo, Mungu akuzidishie baraka na maisha marefu ili mwakani uweze kuchukua tuzo nyingi zaidi. Navutiwa sana na kazi zako dady wetu (akimaanisha yeye na mwanaye).” 

source: Globalpublishers

xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx

Filamu kali ya SIO SAWA inaingia sokoni Ijumaa hii April 2014 hakikisha unanunua nakala yako halisi.
Follow us on twitter Swahili World Planet  and Like our facebook pages Swahili World Planet and Bongomovies SWP for more updates about Swahili movies latest news, gossip, celebrities, features, beauty, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news, life styles news and 

No comments:

Post a Comment