Pages

Thursday, May 29, 2014

Ibuka Na Mil.50 Kama Una Kipaji Cha Kuigiza, Njoo Kwenye Usaili Kesho Makumbusho Ya Taifa Dar.

Baada ya kufanya usaili wa waigizaji wapya mikoani team ya Tanzania Movie Talent(TMT) kesho itafanya usaili wa waigizaji wapya wa filamu wenye vipaji. Kama unacho kipaji huu ndiyo muda wako wa kutoka. Washindi wa mikoani kila mmoja alipewa zawadi ya laki tano na mshindi wa Dar itakuwan hivyo pia halafu washindi wote wa mikoani na Dar watachuana na mshindi wa jumla kujizolea zawadi taslim ya shilingi milioni 50 za kitanzania. Kama wewe upo Dar basi kesho tarehe 30 jitokeze pale makumbusho ya taifa yaliyopo karibu na IFM ujaribu bahati yako na kuibuka na milioni 50 na pia kupata connections kibao katika kiwanda cha filamu Tanzania.

Shindano hilo limeandaliwa na Proin Promotions ambayo ni moja ya kampuni za usambazaji wa filamu Tanzania huku moja wa majaji wakiwa ni Monalisa na Richie
Lulu mmoja wa mastaa wakubwa wa filamu nchini

No comments:

Post a Comment