Monday, May 5, 2014

Diamond Platinumz Atoa Shukrani Kwa Mashabiki Wake Baada Ya Kutwaa Tuzo 7.

Diamond akiwa na Wema Sepetu
Baada ya kung'ara kwa kunyakua tuzo saba katika Kilimanjaro Tanzanian Music Awards 2014, Diamond Platinumz ametoa shukrani kwa kusema "Hakika ilikuwa ni kazi ngumu sana lakini kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu ametufanyia wepesi na hatimaye kufanikisha... Nawashkuru sana sana Mashabiki wangu wote kwakuwa nyie ndio mlionipa tuzo hizi kupitia kura zenu... Family, uongozi wangu.. bila kuvisahau vyombo vyote vya habari vilivyo fanya kazi zangu zisikike kila kona... Niwashukuru pia wasanii wenzangu, kwakuwa naamini wote walifanya kazi nzuri na ndio maana wote tukawa pale ila kwakuwa mshindi ni mmoja, ikatokea kuwa bahati yangu...Ahsanteni sana, cha mwisho ninachoweza kusema tu ni kwamba (Tika! Tika!) yaani (Saba saba) Nomination 7 Tunzo 7...! tuhamieni MTV Awards tuilete Heshima nyumbani sasa"
Diamond akiwa na tuzo alizoshinda

No comments:

Post a Comment