Saturday, April 12, 2014

Steve Nyerere Adaiwa Ni Kuwadi Namba Moja Wa Wasanii Wa Kike, Huwatolea Matusi Ya Nguoni Wakikataa.

Steve Nyerere
Steve Nyerere ambaye ni mwenyekiti wa club ya Bongo Movie Unity amekwaa skendo ya kuwa kuwadi namba moja wa mastaa wa kike nchini kwa viongozi na wafanyabiashara wakubwa. Mmoja wa wasanii wa kike na member wa kundi hilo aliyeonekana kuchukizwa na kitendo hicho akizungumza na Kiu alisema kuwa alikuwadiwa na Steve kwa mfanyabiashara mkubwa mwenye fedha za kutosha "sababu iliyonifanya niongelee jambo hili ni kitendo cha mwenyekiti wetu kuonyesha dharau kwa wasanii wa kike ambapo kwa kiasi kikubwa ndio tunamuweka mjini" alisema msanii huyo

Aliendelea kwa kusema kuwa sababu ya Steve kuwadharau wasanii wa kike ni tangu alipobaini kuwa wasanii wengi wa kundi hilo linalodaiwa kuwa kampuni binafsi ya watu tisa huku wasanii wengine wakifuata mkumbo bila kujua wana elimu kumzidi yeye, inadaiwa kutokana na wasanii anaowaongoza kumzidi kiupeo na kugonga mwamba anapotaka kuwaburuza ndiyo sababu ya kuwadharau. Alisema kuwa mwenyekiti huyo amefikia hatua ya kuwatolea matusi ya nguoni wasanii wa kike wanapokataa kukuwadiwa kwa wafanyabiashara na viongozi anaojuana nao huku akiwasambazia sifa mbaya kwa watayarishaji wa filamu ili kuwaharibia.

Alisema kuwa kama wasichana wa kundi hilo la Bongo movie kama wangekuwa wanajitambua na kukataa kutumiwa basi Steve Nyerere angeishi maisha ya tabu sana hapa mjini. "sababu kubwa ya Steve Nyerere kujuana na viongozi na wafanyabiashara wakubwa ni sisi wasanii wa kike, yeye huwaingia kwa nia ya kuwaunganisha na sisi ili aendeshe maisha yake lakini hana lolote katika uongozi" alisema msanii huyo

Aliendelea zaidi kwa kusema kuwa tangu Steve apate uenyekiti wa kundi hilo basi anajiona kama ameshakuwa mtu muhimu sana katika jamii kumbe kisheria kundi hilo halina mamlaka yoyote kisanaa.

Steve Nyerere alipotafutwa na Kiu na kuelezwa kinagaubaga kuhusu kuwa kuwadi namba moja wa mastaa wa kike alisema kuwa yeye ni jalala ambalo kila aina ya uchafu hutupiwa kwa hiyo hashangai hao watu wanaosambaza habari hizo ambazo zina lengo la kuuchafua uongozi wake ambao anadai umeanza vizuri kwa kutatua matatizo kibao ya wasanii wa kundi hilo ambalo Rais wa Shirikisho La Filamu Tanzania(TAFF) alisema kuwa sio mwanachama wake na pia sio chama bali ni kampuni inayomilikiwa na watu tisa huku wengine wakifuata mkumbo tu. "mimi najenga misingi imara siwezi nikamdharau mtu kwa kuwa ni kiongozi lakini vilevile siwezi kwenda kwenye vibao kata  na kumpigia simu mtu mmoja , hayo ni maneno ya wasanii ambao hawana mashiko katika kuongea na vyombo vya habari" alisema Steve Nyerere.

Ukiachilia mbali hayo wiki kadhaa nyuma baadhi ya viongozi serikalini walikaririwa wakiwalaumu baadhi ya wasanii kuwa ombaomba na wanapoomba wala hawaombi kwa ajili ya kufanya kitu cha maana bali kwa ajli ya kuzidi kuiinua tasnia ya filamu Swahiliwood na badala yake huomba pesa kwa ajili ya kodi au starehe. Katika habari hiyo Jackline Wolper alikuwa mmoja wasanii walioulizwa kuhusu issue hiyo na yeye lijibu kuwa wasanii wanaofanya hivyo wengi ni wanaume na kuonekana ni wasanii wa kike kitu ambacho kinaichafua tasnia nzima ya filamu hata kwa wale wasi na tabia hizo. Steve Nyerere alipoulizwa katika habari hiyo alisema ni kweli suala hilo lipo na yeye binafsi hatoacha kuwapiga mizinga viongozi na wafanyabiashara wakubwa ambao wanazo pesa za kumwaga.


Follow us on twitter Swahili World Planet  and Like our facebook pages Swahili World Planet and Bongomovies SWP for more updates about Swahili movies latest news, gossip, celebrities, features, beauty, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news, life styles news and more

No comments:

Post a Comment