Pages

Saturday, April 5, 2014

Acheni Kutoa Mimba Na Pia Kuzaa Sio Kuzeeka: Batuli

Batuli
Star wa filamu nchini asiye na skendo Yobnesh Yusuph "Batuli" ametoa ushauri kwa wasichana na wanawake wasiopenda kubeba mimba au kutoa mimba hovyo pasipo sababu za msingi. Kupitia mtandao mmoja Batuli amesema .....

"Wasichana, warembo, wadada, wanawake naombeni nilifikishe hili kwenu, binafsi mimi ni mcheza filamu A Kitanzania lakini pia ni mama wa watoto wawili, nimewaita majina mengi tofauti ili walau mnielewe nasema hivi sio kweli kwamba kupata ujauzito, kuwa na watoto ni kujizeesha, acheni kuharibiwa na wenye mitazamo mibovu, acheni kuhatarisha maisha yenu kwa kuua viumbe visivyo na hatia, ikiwa umepata ujauzito kwa bahati mbaya, yaani hukupanga basi mshukuru Mwenyezi Mungu na lea tumbo lako, kumbuka kushika ujauzito nje ya ndoa ni dhambi, Je kushika na kuua kiumbe itakuaje huko uendako? (Siku ya mwisho)" aliandika kwa msisitizo Batuli ambaye ni mama wa watoto wawili huku akiwa na mvuto wa maana kuliko baadhi ya mastaa wenzake wasio na watoto na wanaogopa kuitwa mama kwa kisingizio watazeeka mapema.

                                                                         Batuli
Follow us on twitter Swahili World Planet  and Like our facebook pages Swahili World Planet and Bongomovies SWP for more updates about Swahili movies latest news, gossip, celebrities, features, beauty, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news, life styles news and more

2 comments:

  1. Fact, your right 100% Batuli

    ReplyDelete
  2. Nikimuona Batuli moyo wangu unalipuka lipuka sijui kwanini makofi kwako kwa kuwa mama na bado una mvuto wa ajabu

    ReplyDelete