Pages

Tuesday, March 4, 2014

Wema Sepetu Aumbuka Baada ya Kumdanganya Pastor Myamba Na Kumharibia, Jokate Ajitokeza Na Kumwagiwa Sifa.

Wema Sepetu
Hivi juzi kati Wema Sepetu alialikwa kama mgeni rasmi katika hafla ya chuo cha TFCT cha mafunzo ya filamu kinachomilikiwa na Emmanuel Myamba "Pastor Myamba" ambaye pia ni star wa filamu nchini. Wema alialikwa kwa shinikizo la wanafunzi wa chuo hicho sambamba na Jokate Mwegelo. Wema aliombwa mwanzoni kuhudhuria tukio hilo na kukubali hata hivyo Wema alipopigiwa simu hatua  za mwisho alisema hataweza kufika kwasababu amepata msiba wa shangazi yake. Lakini ikabainika kuwa Wema alimdanganya Myamba kwani hakukuwa na msiba wowote wa shangazi yake kwa mujibu wa chanzo kilicho karibu na Wema kilichozungumza na Globalpublishers, ambapo kilisema kuwa kama kungekuwa na tukio la msiba wangejua tu kwani Wema huwa hawafichi na siku hiyo walikuwa na ratiba ya kwenda kwenye tukio moja la starehe ambalo ratiba yake haikubadilika.

Baada ya tukio la Wema kuikaushia hafla hiyo ilibidi waandaaji wawaombe radhi wageni waalikwa wakiwemo waandishi wa habari, Myamba alipotafutwa na GPL na kuulizwa kuhusu tukio hilo alikiri na kusema amesikitishwa sana na Wema kwa alivyofanya kwani alialikwa kutokana na heshima aliyonayo.
"Nimemshangaa sana lakini mbona mwenzake Jokate alikuja, ni kwasababu anajitambua na ni professional alisema Myamba ambaye alipata umaarufu kwa kuigiza filamu nyingi na marehemu Steven Kanumba akicheza nafasi kama pastor.

                                                                Myamba
Follow us on twitter Swahili World Planet  and Like our facebook pages Swahili World Planet and Bongomovies SWP for more updates about Swahili movies latest news, gossip, celebrities, features, beauty, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news, life styles news and more

No comments:

Post a Comment