Pages

Tuesday, March 18, 2014

Watanzania Hawathamini Mastaa Wao Nitaolewa Na Mwanaume Wa Nje. Jackline Wolper

Star mkubwa wa filamu nchini Jacqueline Wolper ameibuka na kudai kuwa, atafanya kila njia ili aolewe na mwanaume wa nje ya nchi na siyo Wabongo ambao hawathamini mastaa.clip_image001
Akizungumza na Uwazi, Wolper alisema, amefikia uamuzi huo kwa sababu ana uchungu moyoni unaotokana na dhana waliyonayo wanaume wa Kitanzania juu yao, wakiamini kuwa ni wahuni tu hivyo kuwashusha thamani.
 
“Unajua Mtanzania anamchukulia staa kama chombo cha starehe tu na hawezi kumuoa kamwe na hata akimuoa basi hatamthamini kama wanavyothaminiwa wasanii wa huko nje.
clip_image001[7]“Kule bwana (hajataja nchi) mtu akimuoa staa, anampa kipaumbele. Anaweza hata kutumia fedha kuhakikisha anakuwa na staa na maisha ya mke wake yanakuwa yenye amani lakini hapa kwetu tunadharaulika sana ndiyo maana nimefikia uamuzi huu,” alisema Wolper na kuongeza:

“Unajua Watanzania wanaamini staa kuandikwa magazetini ni uhuni lakini wanasahau kuwa maisha yake na magazeti ni kitu cha kawaida kwa sababu ya kujulikana. Mimi sina haja ya kueleza sana lakini naapa kabisa, mimi siwezi kuolewa na Mbongo.”



Follow us on twitter Swahili World Planet  and Like our facebook pages Swahili World Planet and Bongomovies SWP for more updates about Swahili movies latest news, gossip, celebrities, features, beauty, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news, life styles news and more

No comments:

Post a Comment